RAM ni kifupi cha Kiingereza "Random Access Memory" au kumbukumbu isiyo na mpangilio maalumu. Ni aina ya kumbukumbu kwenye kompyuta.

Kadi ra RAM

Hapa programu za kompyuta zina nafasi za kupakua data za kazi zao kwa muda. Programu za kisasa zahitaji nafasi kubwa ya kuhifadhi makadirio kwa muda fulani zikiendelea kukamilisha shughuli. Kadi za RAM zatoa nafasi kupakua data mahali popote bila kujali mpangilio kwanza. Hii huharakisha kazi ya programu.

Sehemu ya RAM inaweza kuwa sehemu kwenye bao kuu lakini kwa kawaida hupatikana kwa kadi ndogo zinazowekwa kwenye bao kuu. Mara nyingi mashine za kompyuta huwa na nafasi ya kuongeza RAM au kubadilisha kadi zake kwa kadi yenye nafasi ya kumbukumbu kubwa zaidi. Kumbukumbu kubwa huwezesha komyuta kutekeleza shughuli zake haraka zaidi.

Kila safari mashine yazimikwa kumbukumbu yote ya RAM yapotea.

RAM isichanganywe na ROM ambayo ni aina tofauti ya kumbukumbu isiyopotea.

pia katika simu Ram ipo na inafanya kazi kama inavyofanya kazi katika komputa, ila huwezi kuiona hivi hivi kwa sababu sio (removable).

Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu RAM kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.