Maajabu ya dunia
Maajabu ya dunia ni orodha ya majengo saba ya pekee iliyojulikana na Wagiriki wa Kale. Wagiriki waliita majengo hayo ΤÀ ΕΠΤÀ ΘΕÁΜΑΤΑ ΤΗΣ ΟΙΚΟΥΜÉΝΗΣ (ΓΗΣ) ta hepta theamata tes oikumenes (ges) - Maajabu saba ya dunia inayokaliwa).
Mara ya kwanza majengo ya ajabu yaliorodheshwa na mwandishi Herodoti mnamo 450 KK. Ilhali maandiko yake hayakuhifadhiwa, habari hii inatokana na waandishi wengine waliomrejea. Kulikuwa na orodha tofauti[1][2] lakini ile inayojulikana na kutajwa zaidi ni ile ya Antipater wa Sidon[3]
Ilhali orodha hii ilikusanywa na waandishi wa Ugiriki ya Kale kuna majengo tu yaliyojulikana katika ustaarabu huo. Kwa hiyo hakuna mifano kutoka Uhindi, China, Asia ya Mashariki, Amerika, Afrika kusini ya Sahara wala Ulaya ya Kaskazini.
Majengo ya orodha ya Antipater hayakudumu hadi leo, isipokuwa Piramidi za Giza. Mengine yaliharibika kutokana na matetemeko ya ardhi au kubomolewa, tena hadi leo hapajulikani mahali pa "Mabustani ya Semiramis". Sanamu na picha za kuchongwa kutoka Kaburi la Mausolo na Hekalu la Artemis zilikusanwa na kuhifadhiwa katika Makumbusho ya Britania mjini London, Uingereza.
Maajabu saba ya Kale
hariri- Piramidi za Giza (Misri ya Kale)
- Mabustani ya Semiramis (Babeli, leo Irak)
- Hekalu ya Artemis mjini Efeso ((Ugiriki ya Kale, leo Uturuki, Asia Ndogo)
- Sanamu ya Zeus mjini Olympia (Ugiriki ya Kale)
- Kaburi la Mausolo mjini Halikarnassos (Ugiriki ya Kale, leo Uturuki)
- Sanamu ya Kolossos kisiwani Rhodos (Ugiriki ya Kale)
- Mnara wa Pharos ya Aleksandria (Misri)
Kati yake piramidi pekee zimebaki hadi leo.
Maajabu ya dunia ya sasa
haririKatika ulimwengu kila siku maajabu yanaongezeka na kufanya maajabu mapya ya dunia kukubalika mara kwa mara. Kwa mfano, mwaka 2016 kuna maajabu yake. Orodha ya maajabu hayo hutolewa na watu mbalimbali kwa mitazamo tofautitofauti: wengine wanaishia upande wa majengo, wengine wanahesabu hata mazuri ya uasilia n.k.
Vitu hivi hadi kufikia kuitwa maajabu ya dunia ina maana ni vya pekee duniani kote, na hakuna kitu kingine kama hicho au cha kufanana nacho.
Tanzania kuna kitu kimoja ambacho kinasemekana ni kati ya maajabu ya dunia ambacho ni kasoko ya Ngorongoro, iliyoko mkoa wa Manyara.
Picha za "Maajabu ya Kisasa"
haririTazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ "History of the Past: World History".
- ↑ Paul Lunde (Mei–Juni 1980). "The Seven Wonders". Saudi Aramco World. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-10-13. Iliwekwa mnamo 2009-09-12.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Antipater, Greek Anthology IX.58
Marejeo
hariri- D'Epiro, Peter, and Mary Desmond Pinkowish, "What Are the Seven Wonders of the World? and 100 Other Great Cultural Lists". Anchor. 1 December 1998. ISBN 0-385-49062-3
- "The Seven Wonders of the World, a History of Modern Imagination" written by John & Elizabeth Romer in 1995
- "The Seven Wonders of the Ancient World" edited by Peter Clayton and Martin Price in 1988
- Johann Conrad Orelli (ed.) Philonis Byzantini Libellus de septem orbis spectaculis. 1816. The original travel guide by Pseudo-Philo
- Lendering, Jona (2007–2010). "Seven Wonders of the Ancient World". Livius.Org. Iliwekwa mnamo 28 Julai 2012.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
hariri- "Seven Ancient Wonders of the World" on The History Channel website. Also includes links to medieval, modern and natural wonders.
- Parkin, Tim, Researching Ancient Wonders: A Research Guide, from the University of Canterbury, New Zealand. – a collection of books and Internet resources with information on seven ancient wonders.
- "Eternal wonder of humanity's first great achievements", by Jonathan Glancey in The Guardian, 10 March 2007
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Maajabu ya dunia kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |