Roald Engebreth Gravning Amundsen (Borge, leo: Fredrikstad, Norwei, 16 Julai 1872 - Aktiki, mnamo 18 Juni 1928) alikuwa mpelelezi Mnorwei aliyekuwa mtu wa kwanza kufika Ncha ya kusini mwaka 1911.

Meli "Belgica" ya Amudsen ikifungwa katika barafu wakati wa safari yake ya kwanza kuelekea Antaktiki mwaka 1898

Kabla ya hapo alikuwa mtu wa kwanza aliyefaulu kuvuka mapito ya kaskazini-magharibi kati ya Atlantiki na Pasifiki katika miaka 1903 - 1906.

Katika safari mbalimbali alikuwa pia mtu wa kwanza aliyevuka Aktiki na ncha ya kaskazini hewani kwa kutumia ndegeputo mwaka 1926.

Alikufa mwaka 1928 kwenye Aktiki alipojaribu kumwokoa mpelelezi Mwitalia aliyekuwa amepotea katika barafu.