Romano wa Kaisarea

Romano wa Kaisarea (alifariki Antiokia, leo nchini Uturuki, 303 hivi) alikuwa shemasi wa Kaisarea Baharini, leo nchini Israeli.

Watakatifu Romano na Barulas walivyochorwa na Francisco de Zurbarán.

Mwanzoni mwa dhuluma ya kaisari Dioklesyano aliteswa kikatili na kukatwa ulimi na hatimaye alinyongwa kwa sababu, alipoona Wakristo kadhaa kutii amri za kaisari huyo na kwenda kuabudu kwenye mahekalu ya miungu, aliwahimiza kwa sauti kubwa washike imara imani yao. [1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadimishwa tarehe 18 Novemba[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.