Sululu-uzuri

(Elekezwa kutoka Rostratula)
Sululu-uzuri
Sululu-uzuri mkubwa
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Charadriiformes (Ndege kama vitwitwi)
Familia: Rostratulidae (Ndege walio na mnasaba na sululu-uzuri)
Jenasi: Nycticryptes Wetmore & Peters, 1923

Rostratula Vieillot, 1816

Sululu-uzuri (au Sururu-uzuri) ni ndege wa jenasi Rostratula na Nycticryptes katika familia Rostratulidae. Wakifanana na sululu, kwa kweli wana mnasaba zaidi na sile-maua. Wana rangi kali kuliko sululu na jike, kama yule wa sile-maua, ni mkubwa na ana rangi kali zaidi kuliko dume ambaye huatamia mayai na kutunza makinda. Wanatokea katika vinamasi na mabwawa ya matete na hutembea wakati wa utusitusi na mwanzo wa usiku. Hula mbegu, wadudu, gegereka, makoa na nyungunyungu. Jike hutaga mayai 2-4 ndani ya tundu juu ya biwi la mimea.

Spishi ya Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri