Rugu ni kata ya Wilaya ya Karagwe katika Mkoa wa Kagera, Tanzania, yenye postikodi namba 35407 [1].

Kata ya Rugu
Nchi Tanzania
Mkoa Kagera
Wilaya Karagwe
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 18,043

Kata ya Rugu inapatikana upande wa Kusini-Mashariki mwa Wilaya ya Karagwe. Hasa inapakana na Ziwa Burigi pamoja na Hifadhi ya Burigi-Chato kwa upande wa Kusini. Mashariki kuna Wilaya ya Muleba, Magharibi ni kata jirani ya Nyakasimbi na Kaskazini ni kata za Nyaishozi (Kaskazini Magharibi) na Ihembe (Kaskazini Mashariki).

Kata ya Rugu ina idadi ya jumla ya vijiji vitano. Vijiji hivyo ni Kasheshe, Misha, Rugu, Ruhita, Misha.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 18,043 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 14,160 waishio humo.[3]

Elimu hariri

Kata ya Rugu ni moja kati ya kata zenye wazazi wanaopenda kuchangia mafanikio ya ukuaji wa elimu ikiwa mwaka 2010 wazazi walichangia kununua vifaa vya sayansi na hivyo kuifanya Shule ya Sekondari Rugu kuwa na maabara mapema sana.

Kata ya Rugu ina shule moja ya sekondari iitwayo Rugu Shule ya Sekondari, na shule nne za msingi ambazo ni Shule ya Msingi: Kasheshe, Misha, Ruhita na Rugu.

Utamaduni hariri

Lugha inayotumiwa na raia wa kata ya Rugu hasa ni Kinyambo (kwa lugha yao: Runyambo).

Marejeo hariri

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01. 
  2. https://www.nbs.go.tz, uk 170
  3. Sensa ya 2012, Kagera - Karagwe-District-Council
  Kata za Wilaya ya Karagwe - Mkoa wa Kagera - Tanzania  

Bugene | Bweranyange | Chanika | Chonyonyo | Igurwa | Ihanda | Ihembe | Kamagambo | Kanoni | Kayanga | Kibondo | Kihanga | Kiruruma | Kituntu | Ndama | Nyabiyonza | Nyaishozi | Nyakabanga | Nyakahanga | Nyakakika | Nyakasimbi | Rugera | Rugu

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rugu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.