Wilaya ya Karagwe
Wilaya ya Karagwe ni wilaya mojawapo kati ya 8 za Mkoa wa Kagera, Tanzania, yenye postikodi namba 35400 [1].
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 332,020 [2] na katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 385,744 [3].
Jina
haririJina Karagwe inasemekana lilitokana na simulizi za wazee mbalimbali na watafiti wa historia ya Karagwe, eti jina linatokana na kilima (ziwa Kitete) kinachopatikana kusini magharibi mwa makao makuu ya wilaya hii, kijiji cha Kandegesho Kwa Omukama (nono ya malija, yaani ukoo wa abhasita)
Wilaya hii inajumlisha sehemu kubwa ya utemi wa Karagwe ya Kale yenye historia ya karne nyingi.
Wilaya ya Karagwe
haririMagharibi ya ziwa Victoria ipo wilaya ya Karagwe na makao makuu ya wilaya hii ni Kayanga, japo kwa sasa imezaa wilaya nyingine ya Kyerwa. Mji huo ni wa zamani na ilijulikana sana ndani na nje ya Tanzania. Uliongozwa sana na Mtemi (Omukama) Rumanyika aliyekuwa na himaya yake huko Bushangaro Bweranyange. Karagwe inapakana na wilaya za Biharamulo, Missenyi na Ngara na inapakana na nchi za Rwanda na Uganda.
Karagwe inakaliwa na kabila la Wanyambo (Abhanyambo) wanaozungumza lugha yao ya Kinyambo (Orunyambo) japo kwa sasa kuna mchanganyiko wa makabila mengi na wageni wengi.
Karagwe ni eneo la kihistoria ya Tanzania ya magharibi upande wa magharibi ya Ziwa Viktoria Nyanza karibu na mpaka wa Burundi. Sehemu kubwa ya eneo hili leo ni wilaya ya Karagwe katika Mkoa wa Kagera.
Karagwe ya leo imetoka mbali na kila kizazi kinachozuka kinaongeza yake juu ya Karagwe na wao wenyewe.
Watawala wa Karagwe
haririWatawala wa Karagwe walikuwa na cheo cha "Umugabe". Nasaba ilianzishwa mnamo mwaka 1450 na mtemi Ruhinda I aliyeitwa pia Bunyambo.
1675 - 1700 Ruhinda V
1700 - 1725 Rusatira
1725 - 1750 Mehinga
1750 - 1775 Kalemera I Ntagara Bwiragenda (alifariki 1775)
1775 - 1795 Ntare V "Kiitabanyoro"
1795 - 1820 Ruhinda VI Orushongo "Lwanyabugondo" (b. 1777 - d. 1820)
1820 - 1853 Ndagara I "Luzingamcucu lwa nkwanzi"
1853 - 1881 Rumanyika I Rugundu
1882 - 1886 Ndagara II Nyamkuba
1886 - 1893 Kalemera II Kanyenje
1886 - 1893 Kakoko -Regent
1893 - 1914 Ntare VI
1914 - 1916 Kahigi -Regent
1916 - 1939 Daudi Rumanyika II
1939 - 1962 - 9.12. B. Itogo Ruhinda VII
Marejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
- ↑ Sensa ya 2012, Kagera - Karagwe-District-Council
- ↑ https://www.nbs.go.tz
Kata za Wilaya ya Karagwe - Mkoa wa Kagera - Tanzania | ||
---|---|---|
Bugene | Bweranyange | Chanika | Chonyonyo | Igurwa | Ihanda | Ihembe | Kamagambo | Kanoni | Kayanga | Kibondo | Kihanga | Kiruruma | Kituntu | Ndama | Nyabiyonza | Nyaishozi | Nyakabanga | Nyakahanga | Nyakakika | Nyakasimbi | Rugera | Rugu |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Karagwe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |