Ruth Meena

Mwanaharakati na mwalimu wa haki za wanawake wa Tanzania

Ruth Meena(alizaliwa mwaka 1946) ni Mtanzania mwanaharakati na mwalimu kwa miongo mitatu katika ngazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na sekondari, vyuo vya ualimu na chuo kikuu.

Ruth Meena
Amezaliwa 1946
Kiwalaa Mbokomu
Nchi Tanzania
Kazi yake Mwanaharakati na mwalimu

Alikuwa Profesa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambako alihudumu katika Idara ya Sayansi ya Siasa kwa takribani miaka 30.

Alistaafu kazi yake ya chuo kikuu miaka michache iliyopita na kuanzisha shule ya Raida High School na Kituo cha Kujifunza, anavyovisimamia.

Pia ni mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa wanawake Tanzania.[1] na ni mmoja wa waandishi ya makala iitwayo Women and Political Leadership: Facilitating Factors in Tanzania [2]

Ruth Meena alishirikiana na UNRISD kama sehemu ya timu ya utafiti wa Tanzania kwa mradi wa UNRISD juu ya Uchumi wa Kisiasa na Jamii.[3]

Maisha ya awali hariri

Profesa Meena alizaliwa katika familia yenye watoto kumi na wawili, wasichana kumi na wavulana wawili.

Dada yake mkubwa alipoolewa, Meena (akiwa na umri wa miaka mitano) alienda kulelewa kwa dada yake.[4]

Mwaka wa 1968 Profesa Meena alikuwa miongoni mwa wanawake wachache waliochaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki, ambacho mwaka 1971 kilibadilishwa na kuitwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo alihitimu. [5]

kazi hariri

[6]


Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ruth Meena kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.