Safu ya Ruwenzori

safu ndogo ya milima katikati mwa Afrika, iliyoko kwenye mpaka kati ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
(Elekezwa kutoka Rwenzori)

Safu ya Ruwenzori (pia: Rwenzori) ni eneo la milima katika Afrika ya Kati kwenye mpaka wa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Safu ya Rwenzori kusini kwa Fort Portal (Uganda).
Mimea ya pekee ya Rwenzori.

Mlima wa juu ni Pic Marguerite (Mlima Stanley) wenye kimo cha mita 5,109 juu ya UB. Mingine ni mlima Speke (m 4,890), mlima Baker (m 4,844), mlima Emin (m 4,798), mlima Gessi (m 4,715) na mlima Luigi di Savoia (m 4,627).

Baada ya Kilimanjaro na mlima Kenya, Ruwenzori ni mlima mkubwa wa tatu barani Afrika. Pamoja na hiyo miwili ndiyo milima pekee yenye barafuto za kudumu kwenye bara hilo.

Huaminiwa ya kwamba Rwenzori ni ile "Milima ya Mwezi" iliyotajwa katika taarifa za Klaudio Ptolemaio zamani za Misri ya Kale.

Tazama pia hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Safu ya Ruwenzori kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.