Salaberga
Salaberga (labda Toul, leo nchini Ufaransa, 605; Laon, leo nchini Ufaransa, 670 hivi) alikuwa mwanamke wa ukoo wa kifalme ambaye, baada ya kuolewa mara mbili na kuzaa watoto watano, alikubaliana na mume kutawa, naye alianzisha monasteri dabo akawa abesi wake.
Inasemekana Kolumbani alimponya upofu akamwelekeza kumtumikia Mungu[1].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, sawa na mumewe wa pili, Blandinus, na watoto wao wawili, Baldwini na Anstrudis.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Septemba[2].
Tazama pia
haririTanbihi
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |