Samos ni kisiwa cha Ugiriki kilichopo kilomita 1.3 mbele ya pwani ya Uturuki. Ni pia moja ya wilaya 51 za Ugiriki.

Mahali pa Samos.

Samos ina urefu wa km 44 na upana wa km 19; eneo lake ni km² 477. Sehemu kubwa ni milima inayofikia kimo cha mita 1,153 juu ya usawa wa bahari.

Kuna wakazi 33,800 na mji mkubwa, unaoitwa Samos vilevile, una watu 6,000.

Uchumi unategemea utalii pamoja na kilimo. Divai ya Samos ni maarufu.

Katika historia ya Ugiriki ya Kale Samos ilikuwa nyumbani kwa wataalamu mashuhuri kama Pythagoras, Epikuri, Herodoti na Aristarko wa Samos.

Mahali kadhaa pameorodheshwa na UNESCO kama Urithi wa Dunia.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ugiriki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Samos kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.