Severo wa Viza (alifariki Viza, Tracia, katika Uturuki ya leo, 304 hivi) alikuwa Mkristo aliyeuawa kwa ajili ya imani yake wakati wa dhuluma ya makaisari Diokletian na Maximian.

Akitamani kufia dini, aliongoa akida Memno wa Viza ambaye, kisha kuteswa kikatili pamoja naye, alimtangulia kuuawa[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Julai[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.