Sevilla FC
Sevilla Fútbol Club ni kilabu ya mpira wa miguu ya nchini Hispania iliyo na makao yake makuu huko Seville, mji mkuu na jiji kubwa zaidi la jamii inayojitegemea ya Andalusia, Uhispania . Inacheza katika ligi kuu ya soka la Uhispania, La Liga . Sevilla wameshinda ligi ya UEFA Europa mara sita, idadi kubwa kuliko klabu yoyote duniani. [1] Ni klabu kongwe zaidi ya mchezo wa mpira nchini Uhispania. [2] [3] [4] [5] Klabu hii iliundwa tarehe 25 Januari 1890, [2] [3] [4] [5] huku mzaliwa wa Uskoti Edward Farquharson Johnston akiwa rais wao wa kwanza wa klabu hio. Tarehe 14 Oktoba 1905, makala ya ushirika ya klabu hio ilisajiliwa katika Serikali ya Kiraia ya Seville chini rais mzaliwa wa Jerez,José Luis Gallegos Arnosa. Sevilla ina ushindani wa muda mrefu na wapinzani wa mji mikubwa wa Real Betis .
Sevilla pia ndiyo klabu iliyofanikiwa zaidi kwenye kandanda Andalusia kwa suala la kuchukua mataji, ikiwa na Vikombe kumi na nane vya Andalusia, [6] taji moja la ligi la kitaifa mnamo 1945-46, mataji matano ya Kombe la Uhispania ( 1935, 1939, 1948, 2007 na 2010 ), moja la Uhispania na la Super Cup ( 2007 ), rekodi sita za makombe ya UEFA /UEFA Europa ( 2006, 2007, 2014, 2015, 2016 na 2020 ) na UEFA Super Cup moja ( 2006 ). Pia waliteuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Historia ya Soka na Takwimu kama klabu bora zaidi ya Dunia mwaka 2006 na 2007, hivyo kuwa klabu ya kwanza kufikia kupewa nafasi hii katika miaka miwili mfululizo. [7]
Vilabu vya mashabiki
haririVilabu vya mashabiki wa Sevilla vimejikita zaidi katika jiji la Seville, jimbo lake na maeneo mengine ya Andalusia. Uwepo wa vilabu vya mashabiki katika jumuiya nyingine zinazojitegemea ni mkubwa zaidi katika miji ya Catalonia na Extremadura . Wengi wao wamejumuishwa katika "Shirikisho la Vilabu vya Mashabiki wa San Fernando" (Federación de Peñas Sevillistas "San Fernando"), ambalo shirika hilo, kulingana na sheria zake, ni huru kabisa kutoka kwenye bodi ya klabu, kuwa na bodi yake na isiyoingiliwa na chama ama klabu yoyote.
Upinzani
haririSevilla wanachuana kwenye dabi ya Seville dhidi ya wapinzani wao wa jiji la kati Real Betis . Wawili hao walicheza kwa mara ya kwanza tarehe 8 Oktoba 1915 katika mechi ambayo ilisha kwa Sevilla 4-3. Mchezo huo unachukuliwa kuwa moja ya dabi muhimu zaidi katika kandanda ya nchini Uhispania . Sevilla pia ina upinzani mkubwa na klabu ya mpira ya Atlético Madrid na Valencia CF.
Marejeo
hariri- ↑ UEFA.com. "Most titles | History | UEFA Europa League". UEFA.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-06-20.
- ↑ 2.0 2.1 "Your BNA Stories: Sevilla Football Club – the Oldest Football Club in Spain, Founded in 1890 by British Residents". The British Newspaper Archive. 5 Oktoba 2012.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 "Courier proves Seville's claim as Spain's oldest football club". The Courier. 7 Februari 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Februari 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 4.0 4.1 "The day Spanish football was born". Marca. 9 Oktoba 2012.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 5.0 5.1 "How Glasgow man Hugh McColl helped set up Spain's oldest football club". Evening Times. 11 Oktoba 2012.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Honours". sevillafc.es. Iliwekwa mnamo 2022-01-03.
- ↑ "El Sevilla, premio de la IFFHS al mejor equipo del pasado año".