Shirika la Huduma kwa Wanyama Pori ya Kenya
Shirika la Kenya la Wanyama Pori (KWS - Kenya Wildlife Service) lilianzishwa mwaka 1990. Inasimamia uasilia na viumbe hai wa nchi, ikilinda na kuhifadhi flora na fauna.
KWS inasimamia mbuga za wanyama za kitaifa na hifadhi nchini Kenya. Fedha zinazokusanywa kama ada ya kiingilio hutumika kusaidia uhifadhi wa mimea na wanyama ndani ya hifadhi au mbuga.
Mbuga za Kitaifa na za Hifadhi
haririKenya ina mbuga na hifadhi 35 teule za kitaifa:
- Hifadhi ya Taifa ya Aberdare
- Hifadhi ya Taifa ya Amboseli
- Hifadhi ya Taifa ya Arabuko Sokoke
- Hifadhi ya Taifa ya Arawale
- Hifadhi ya Taifa ya Bisanadi
- Hifadhi ya Taifa ya Boni
- Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Kati
- Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Chyulu
- Hifadhi ya Taifa ya Hell's Gate
- Hifadhi ya Msitu wa Kakamega
- Hifadhi ya Majini ya Kisite-Mpunguti
- Hifadhi ya Paa ya Kisumu
- Hifadhi ya Taifa ya Kora
- Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Nakuru
- Hifadhi ya Taifa ya Losai
- Hifadhi ya Taifa ya Majini ya Malindi
- Hifadhi ya Taifa ya Malka Mari
- Hifadhi ya Taifa ya Marsabit
- Hifadhi ya Taifa ya Meru
- Hifadhi ya Majini ya Mombasa
- Hifadhi ya Taifa ya Mlima Elgon
- Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kenya
- Hifadhi ya Taifa ya Mlima Longonot
- Hifadhi ya Taifa ya Mwea
- Hifadhi ya Taifa ya Nairobi
- Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Ndere
- Hifadhi ya Taifa ya Ol Donyo Sabuk
- Hifadhi ya Taifa ya Ruma
- Hifadhi ya Taifa ya Saiwa Swamp
- Hifadhi ya Taifa ya Samburu
- Hifadhi ya Taifa ya Shaba
- Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Shimba
- Hifadhi ya Taifa ya Sibiloi
- Hifadhi ya Nyani ya Mto Tana
- Hifadhi ya Taifa ya Tsavo Mashariki
- Hifadhi ya Taifa ya Tsavo Magharibi
- Hifadhi ya Majini ya Watamu
Mipango ya Uhifadhi
haririKWS inaendesha mipango maalum kusaidia viumbe na makazi ya Kenya ambayo yako kwenye hatari hasa. Wana mipango ya uhifadhi wa sehemu za chemchemi na misitu,na miradi maalum ya tembo na kifaru kusaidia kuwaokoa kutoka kwa wawindaji. Hirola, ambayo iko katika hatari ya kupotea, pia inafuatiliwa.
Ndani ya KWS kuna huduma kadhaa, kila moja ikiwajibika kwa eneo tofauti la kazi:
Huduma ya Wanyama Pori ya Jamii
haririHili tawi la KWS hufanya kazi nje ya hifadhi za taifa. Wao badala hufanya kazi katika maeneo kama vile kanda za wanyamapori, na kufundisha jamii wanaoishi huko kuhamasisha uhifadhi na kuchunga rasilimali zao.
Huduma za Usalama
haririKazi ya huduma hii ni kuondoa uwindaji katika hifadhi za kitaifa, na kukomesha biashara haramu.
Huduma za Matibabu ya Wanyama
haririHuduma hii huhakikisha kuwa afya ya kuzaliana ya wakazi wa aina inazingatiwa kote nchini.
Mafunzo
haririKWS ina kituo cha mafunzo mjini Naivasha. Watumishi wa KWS hufundishwa hapa, na pia mafunzo kwa wanafunzi wa nje wa ikolojia na utalii.
Elimu
haririKWS inendesha vituo kadhaa vya elimu:
- Nairobi Safari Walk
- Kituo cha Elimu cha Nairobi
- Kituo cha Elimu cha Ziwa Nakuru
- Kituo cha Elimu cha Tsavo Mashariki
- Kituo cha Elimu cha Tsavo Magharibi
Hizi ziko ndani ya Hifadhi za Taifa, na huendesha mipango ya kuhamasisha watu kuhudumia na kulinda mazingira yao. Imelengwa kwa wananchi, hasa makundi ya shule, lakini ni wazi kwa mtu yeyote.
Angalia pia
haririMarejeo
haririViungo vya nje
hariri- Shirika la Huduma kwa Wanyama Pori ya Kenya Ilihifadhiwa 14 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine.