Shirikisho la Ujerumani Kaskazini
Shirikisho la Ujerumani Kaskazini (kwa Kijerumani: Norddeutscher Bund) [1] lilikuwa maungano ya madola 22 ya Kijerumani chini ya uongozi wa Ufalme wa Prussia.
Kwa miaka michache ilichukua nafasi ya Shirikisho la Ujerumani lililofutwa mwaka 1866 likawa mtangulizi wa Dola la Ujerumani lililoundwa mwaka 1871.
Lilitanguliwa kwenye Agosti 1866 na ushirikiano wa kijeshi kati ya Prussia na madola madogo jirani baada ya ushindi wa Prussia juu ya Austria katika Vita ya Kijerumani ya 1866. Tangu tarehe 1 Julai 1867 ilikuwa na katiba iliyoifanya shirikisho la madola katika Ujerumani upande wa kaskazini wa mto Main.
Shirikisho hilo lilidumu hadi Januari 1871 wakati lilipoingia katika Dola la Ujerumani lililoundwa baada ya ushindi juu ya Ufaransa katika vita ya 1870/71. Dola hilo liliunganisha Shirikisho la Ujerumani Kazkazini pamoja na madola ya Ujerumani Kusini kama vile Bavaria, Baden na Wurttemberg.
Shirikisho hilo lilidumu miaka 3 na nusu pekee lakini katiba yake ilikuwa baadaye pia katiba ya Ujerumani iliyounganishwa tangu 1871. Mfalme wa Prussia alikuwa rais wa shirikisho. Sheria zilipitishwa na Bunge la Shirikisho (Reichstag) lililochaguliwa kwa kura za raia wote wa kiume na Halmashauri ya Shirikisho walipokutana wawakilishi wa serikali za madola.[2]
Shirikisho lote lilikuwa na wakazi milioni 30, na kwa asilimia 80 waliishi katika majimbo ya Prussia.
Orodha ya madola wanachama
haririMarejeo
haririKujisomea
hariri- Craig, Gordon A. Germany, 1866–1945 (1978) pp. 11–22 online edition Archived 12 Agosti 2011 at the Wayback Machine.
- Holborn, Hajo (1959). A History of Modern Germany: 1840–1945. ku. 173–232. ISBN 9780394302782.
- Hudson, Richard. "The Formation of the North German Confederation." Political Science Quarterly (1891) 6#3 pp: 424–438. in JSTOR
- Nipperdey, Thomas. Germany from Napoleon to Bismarck: 1800-1866 (1996), very dense coverage of every aspect of German society, economy and government
- Pflanze, Otto. Bismarck and the Development of Germany, Vol. 1: The Period of Unification, 1815–1871 (1971)
- Taylor, A.J.P. Bismarck: The Man and the Statesman (1967) online edition Archived 24 Juni 2011 at the Wayback Machine.