Shota Rustaveli

Shota Rustaveli (1172 - 1216) alikuwa mshairi nchini Georgia wakati wa karne ya 12. Hutazamiwa kama mwanzilishaji wa fasihi ya Kigeorgia isiyo ya kidini.

Shota Rustaveli - picha kwenye ukuta wa kanisa alikozikwa

Utenzi wake unaojulikana zaidi ni "Mshujaa anayevaa ngozi ya chui" ni utenzi mwenye beti 1,550 uliosimuliwa tangu siku za mshairi mwenyewe na Wageorgia wakiwa na sherehe au sikukuu.

MaishaEdit

Hakuna uhakika juu ya maisha yake lakini habari za kale kutoka Georgia zasema yakwamba alipata elimu nzuri nchini Georgia na baadaye Ugiriki yaani katika Milki ya Bizanti. Anaaminiwa alikuwa waziri wa malkia wa Georgia hata mpenzi wake alipaswa kuondoka nchini wakati malkia alipoolewa akahamia Yerusalemu. Hapa alijitolea kupamba na kutengeneza monasteri ya Msalaba Mtakatifu mjini Yerusalemu alikozikwa. Uchoraji wa ukutani unamkumbuka hadi leo.


Kazi yakeEdit

 
Ukurasa wa utenzi wake

"Mshujaa anayevaa ngozi ya chui" imetafsiriwa katika lugha nyingi. Ilichapishwa mara ya kwanza mjini Tbilisi mwaka 1712.

Tovuti za NjeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shota Rustaveli kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.