Silvano wa Gaza na wenzake

Silvano wa Gaza na wenzake 39 (alifariki katika migodi ya shokoa ya Mismiya, Palestina, 311) alikuwa askofu wa Gaza hadi kifodini alichopata pamoja na hao wenzake kwa kukatwa kichwa chini ya kaisari Maximinus Daia[1] [2] [3].

Mt. Silvano wa Gaza katika mchoro mdogo, Ado, Martyrologium et obituarium. karne ya 12, Bibliothèque nationale de France (côte Latin 17767 [ff. 11-166]).

Eusebi wa Kaisarea aliandika habari za mateso yao[4].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa katika tarehe 4 Mei[5].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.