Simona Marchini (alizaliwa Roma, 19 Desemba 1941) ni mwigizaji, mtangazaji wa redio na runinga, muongozaji wa jukwaa, mchekeshaji na anajihusisha na sanaa nchini Italia.

Simona Marchini
Amezaliwa19 Desemba 1941
UtaifaItalia
Kazi yakeMchekeshaji
WatotoRoberta Paolopoli

Maisha na Kipaji chake hariri

Alizaliwa na mfanyabiashara anayeitwa Alvaro, alihitimu shahada yake ya fasihi katika chuo kikuu cha La Sapienza.[1]

Anapenda sanaa, tangu mwaka 1966 aliongoza nyumba kadhaa za sanaa, moja ya nyumba ya sanaa aliyoiongoza ni "Nuova Pesa" na aliongoza nyumba hiyo kati ya mwaka 1985 na 1995.[1][2]

Baada ya kuwa mwigizaji na muongozaji hodari, mwaka 1980 alianza uchekeshaji katika maonyesho tofauti tofauti kwenye runinga RAI A tutto gag na alionekana katika baadhi ya filamu za uchekeshaji, televisheni na vipindi vya redio.

Maisha yake binafsi hariri

Aliwahi kuolewa na mwanamume kutoka familia tukufu Calabria, na 1970 mpaka 1980 Marchini aliolewa na mchezaji wa mpira Franco Cordova.[2]

Marchini pia ni balozi wa UNICEF UNICEF Goodwill Ambassador.[2]

Marejeo hariri

  1. 1.0 1.1 Enrico Lancia, Roberto Poppi. Dizionario del cinema italiano, Le Attrici. GremeseEditore, 2003. ISBN 888440214X. 
  2. 2.0 2.1 2.2 Giorgio Dell’Arti, Massimo Parrini. Catalogodeiviventi. Marsilio, 2009. ISBN 9788831795999.
  Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Simona Marchini kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.