Daa-njugu

(Elekezwa kutoka Sipuncula)
Daa-njugu

Daa-njugu (Themiste petricola). Juu: mwili umefupishwa (umbo la njugu); chini: mwili umerefuka.
Daa-njugu (Themiste petricola).
Juu: mwili umefupishwa (umbo la njugu); chini: mwili umerefuka.
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Nusuhimaya: Eumetazoa
Faila ya juu: Lophotrochozoa
Faila: Sipuncula
Rafinesque, 1814
Ngazi za chini

Ngeli 2, oda 4:

Daa-njugu (kutoka kwa Kiing. peanut worm) ni wanyama wadogo wa faila Sipuncula wanaofanana na daa wa kawaida. Jina linatoka kwa umbo lao la njugu wakiwa wamejifupisha.

Daa-njugu hutofautiana kwa ukubwa lakini spishi nyingi zina urefu wa chini ya sm 10. Mwili umegawanywa katika kiwiliwili kinene kisicho na pingili na sehemu nyembamba ya mbele ambayo inaweza kurudishwa ndani ya kiwiliwili. Mdomo uko kwenye ncha ya sehemu hii ya mbele na umezungukwa katika vikundi vingi kwa duara ya minyiri mifupi. Kwa sababu hauna sehemu ngumu, mwili ni kinamo. Ingawa hupatikana katika anuwai ya makazi katika bahari zote za dunia spishi nyingi huishi katika makazi ya kina kifupi, wakichimba chini ya uso wa sakafu za mchanga na matope. Nyingine zinaishi chini ya mawe, katika mianya ya miamba au katika maeneo mengine yaliyofichwa.

Daa-njugu wengi hujilisha kwa mabaki madogo wakirefusha mwili wa mbele ili kukusanya chembe za chakula na kuzivuta kinywani. Inarudishwa wakati hali ya kujilisha haifai au hatari inatishia. Isipokuwa spishi chache, uzazi ni wa kijinsia na unahusisha hatua ya lava wa kiplanktoni. Daa-njugu hutumiwa kama chakula katika baadhi ya nchi za Asia ya Kusini-Mashariki.