Stadi za maisha
Stadi za maisha ni maarifa yanayotarajiwa kumsaidia mtu kuishi vema[1] .
Ufafanuzi
haririMaisha ni muambatano wa muda pamoja na matukio, hivyo ni muhimu kufahamu kuwa muda unavyozidi kwenda ndipo kiumbehai kinapopata nafasi ya kupita katika matukio mbalimbali yaliyo mazuri na mabaya, amayo yote huhitaji hekima na maarifa katika kuyapitia hususan yaliyo mabaya.
Kuna msemo wa lugha ya Kiswahili unaosema kuwa "Kuishi kwingi ni kuona mengi": maana halisi ni kuwa mtu aliyemtangulia mwenzake kiumri anakuwa na uzoefu mkubwa sana kwa sababu mambo ambayo amekwisha kuyaona ni mengi katika kuishi kwake. Kupitia uzoefu huo ndivyo mtu huyo anapata mbinu nyingi za kumwezesha yeye kukabiliana na nyakati zote katika maisha yake.
Haina maana ya kwamba mtu mwenye umri mdogo, kwa sababu ya kuwa na uzoefu mdogo wa kimaisha, basi anapaswa kukosa busara na hekima za kumwezesha yeye kuishi vizuri.
Mtoto au kijana anaweza kuwa na hekima kama ya mzee kwa kujifunza stadi za maisha ambazo ni kama zifuatazo[2]:
- Stadi binafsi
- Stadi za kijamii
- Stadi za maamuzi sahihi[3]
Stadi binafsi
haririHizi ni mbinu au kanuni ambazo zinamwezesha mhusika kuwa na uwezo mkubwa wa kujitambua, kwanza kiundani zaidi, kwa maana ya hisia, uwezo, madhaifu na nafasi yake katika jamii. Stadi binafsi ni muhimU sana kwa sababu zinamwezesha mhusika huyo kujijengea hali ya kujiamini kutokana na kuitambua thamani yake katika jamii inayomzunguka.
Ili kuwa bora katika stadi binafsi mhusika anapaswa kuwa na uwezo katika vitu vifuatavyo: kujitambua, kutambua mahitaji na kuweka malengo katika maisha.
Stadi za kijamii
haririHizi ni stadi ambazo humjenga na kumwezesha mhusika kujua naamna ya kuishi na watu kwa upendo na amani na kujenga ushirikiano ulio bora. Vifuatavyo ni vipengele muhimu ambavyo vinamthibitisha mtu kuwa stadi za kijamii:
- uwezo wa kujenga mahusiano mazuri na watu wanaomzunguka
- uwezo wa kujitawala kifikra na kuepuka misukumo hasi
- uwezo wa kutambua na kujihusisha katika kusaidia changamoto za wanajamii
- mawasiliano mazuri
Stadi za maamuzi sahihi
haririHizi ni stadi ambazo zinamwezesha mhusika kufanya maamuzi sahihi wakati wa changamoto na yanapotokea machaguo mengi. Kama ilivyo katika stadi nyingine hizi pia zina kanuni ambazo ndizo msingi wa kupatikana kwa maamuzi sahihi, nazo ni kama ifuatavyo.
- mawazo chanya
- ubunifu wa kimawazo
- maono ya mbeleni
- uwezo wa kufanya maamuzi
Vyanzo vya stadi za maisha
haririWatu hujifunza/kuiga stadi za maisha katika sehemu, makundi au watu mbalimbali ila sehemu au vitu ambavyo ndio msingi wa stadi za maisha ni hizi zifuatazo.
Familia zetu
haririHapa tunajifunza na kuiga vitu kutoka kwa wazazi au ndugu zetu kwa sababu tunaishi nao kwa muda mreefu, hususani katika kipindi cha ukuaji wetu ambacho ndicho kipindi vichwa vyetu vinapodaka na kukariri mambo mengi[4].
Taasisi za kielimu
haririHapa mara nyingi ni kupitia maarifa tunayopata kwa kufundishwa na wakufunzi hususadi shuleni, vyuoni na kadhalika.
Jamii zetu
haririTofauti na familia kuna kundi jingine kubwa ambalo linatuzunguka, hivyo lenyewe pia lina mchango katika kutujenga kifikra na kuendeleza stadi zetu za kimaisha.
Imani/Dini
haririImani tofautitofauti zimekuwa zikitoa mafunzo mengi ya kidini ambayo yamekuwa yakihusika katika kuwajenga waumini wake. Kwa mfano imani ya Kikristo imekuwa ikifundisha juu ya amri kuu ya upendo, kitu ambacho ni stadi muhimu inayowezesha mtu kuishi vizuri na watu katika jamii yake.
Tanbihi
hariri- ↑ Life Skills Education for Children and Adolescents in Schools (Ripoti). World Health Organization. Iliwekwa mnamo 29 Desemba 2020.
{{cite report}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Skills & Competencies - CASEL". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Mei 2011. Iliwekwa mnamo 10 Juni 2018.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); More than one of|archivedate=
na|archive-date=
specified (help); More than one of|archiveurl=
na|archive-url=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Global evaluation of life skills education programmes". unicef.org (Evaluation Report). New York: United Nations Children’s Fund. 17 Novemba 2016. ku. 8–9. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-06-02. Iliwekwa mnamo 29 Desemba 2020.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Prinz, Ron (2009). "Behavioral parent training". Encyclopedia of Human Relationships. doi:10.4135/9781412958479.n53. ISBN 9781412958462.
Marejeo
hariri- People Skills & Self-Management (free online guide) Ilihifadhiwa 2 Juni 2021 kwenye Wayback Machine., Alliances for Psychosocial Advancements in Living: Communication Connections (APAL-CC)
- Reaching Your Potential: Personal and Professional Development, 4th Edition
- Andrew J. DuBrin (2016). Human Relations for Career and Personal Success: Concepts, Applications, and Skills. Pearson Education. ISBN 978-0-13-413171-9.
- Life Skills: A Course in Applied Problem Solving., Saskatchewan NewStart Inc., First Ave and River Street East, Prince Albert, Saskatchewan, Canada.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Stadi za maisha kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |