Stefano wa Grandmont

Stefano wa Grandmont (kwa Kifaransa: Étienne de Muret; Thiers, Auvergne, Ufaransa, 1045 - Muret, Limoges, Ufaransa, 8 Februari 1124) alikuwa padri halafu abati wa shirika la kimonaki alilolianzisha huko Grandmont kwa kufuata maisha magumu na fukara sana[1][2]. Alipanga waklero wajitose katika maisha ya sala tu na mabradha wawajibike katika shughuli nyingine zote.

Mt. Stefano alivyochorwa katika karne ya 12 akiwa na Hugh Lacerta.

Alitangazwa na Papa Klementi III kuwa mtakatifu mwaka 1189.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Februari[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/40000
  2. His works (not authentic) may be found in Migne, P. L. CCIV, 997-1162.
  3. Martyrologium Romanum
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.