Mlangobahari wa Otranto

(Elekezwa kutoka Strait of Otranto)

Mlangobahari wa Otranto (kwa Kiingereza: Strait ya Otranto) unaunganisha Adria na Bahari ya Ionia. Unatenganisha Italia na Albania. Upana wake karibu na Salento ni chini ya kilomita 72. [1] Jina linatokana na mji wa Italia wa Otranto.

Ramani inayoonyesha eneo la Mlangobahari wa Otranto.

Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, mlango huo ulikuwa na umuhimu wa kimkakati. Wanamaji wa ushirikiano wa Italia, Ufaransa, na Uingereza walizuia manowari za Austria-Hungaria kutoka kwenye Adria na kuingia Bahari ya Mediteranea .

Marejeo

hariri
  1. Cushman-Roisin, Benoit; Gacic, Miroslav; Poulain, Pierre-Marie; Artegiani, Antonio (2001). Physical Oceanography of the Adriatic Sea: Past, Present and Future. Springer Netherlands. uk. 93. ISBN 978-1-4020-0225-0.
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mlangobahari wa Otranto kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.