Bahari ya Ionia (kwa Kigiriki Ιόνιο Πέλαγος ionio pelagos; kwa Kiitalia Mar Ionio; kwa Kialbania: Deti Jonë; kwa Kiingereza: Ionian Sea) ni sehemu ya Bahari Mediteranea upande wa kusini wa Bahari ya Adria.

Ramani ya eneo hilo.

Inapakana na Italia ya kusini (mikoa ya Puglia, Basilicata, Calabria na Sisilia) upande wa magharibi, Albania na Ugiriki upande wa mashariki.

Jina hariri

Jina linatokana na Io, mhusika katika mitholojia ya Ugiriki ya Kale. Io alikuwa mpenzi wa kibinadamu wa mungu Zeus, alivuka bahari hiyo. Hakuna uhusiano na nchi ya kihistoria ya Ionia iliyokuwepo kwenye pwani ya Anatolia (rasi ya nchini Uturuki), upande wa mashariki ya Ugiriki, ilhali Bahari ya Ionia iko upande wa magharibi ya Ugiriki. Kwa alfabeti ya Kigiriki kila "ionia" huandikwa kwa herufi ya "o" tofauti (Ιόνιο - Ἰωνία).

Visiwa hariri

Kuna visiwa vingi upande wa mashariki wa sehemu hii ya bahari na vyote ni sehemu ya Ugiriki: Korfu, Zakynthos, Kefalonia, Ithaka na Lefkada.

Visiwa vichache vidogo viko pia upande wa Italia.

Usafiri hariri

Kuna usafiri kwa feri baina ya bandari ya Patras na Igoumenitsa upande wa Ugiriki, halafu Brindisi na Ancona upande wa Italia.

  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bahari ya Ionia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.