Tamaro wa Benevento
Tamaro wa Benevento (alifariki 490 hivi) alikuwa askofu wa mji huo wa Italia Kusini lakini alikuwa mzaliwa wa Afrika Kaskazini.
Baada ya kuteswa na Wavandali Waario kwa sababu ya imani yake, alifukuzwa akiwa na wenzake 12, wakiachwa baharini katika meli mbovu isiyoweza kuendeshwa.
Labda wakati huo alikuwa padri au askofu tayari. Inasemekana pia alikuwa mfuasi wa Augustino wa Hippo.
Baada ya kufika Italia, aliishi kama mkaapweke, lakini alitafutwa aongoze jimbo.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Septemba.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |