Tegu
Tegu wa nguruwe (Taenia solium)
Tegu wa nguruwe (Taenia solium)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Nusuhimaya: Eumetazoa
(bila tabaka): Bilateria
(bila tabaka): Prostomia
Faila ya juu: Platyzoa
Faila: Platyhelminthes
Ngeli: Rhabditophora
Nusungeli: Trepaxonemata
Oda: Cestoda
Ngazi za chini

Nusuoda 2 na oda za chini 18

Mategu ni aina za minyoo yaliyo bapa (minyoo-bapa) katika oda Cestoda na faila Platyhelminthes. Mategu waliokomaa huishi kama vidusia katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula wa vertebrata ambapo hufyunda virutubishi katika giligili ya utumbo. Lava wa takriban spishi zote hukua katika spishi nyingine ya mwenyeji kuliko yule wa wazazi na mara nyingi katika arithropodi. Wenyeji wakubwa wana spishi kubwa za mategu, k.m. Polygonoporus giganticus wa nyangumi ana urefu wa m 30, na wenyeji wadogo wana mategu wadogo, k.m. Vampirolepis murini wa virukanjia ana urefu wa mm 8-15. Tegu anayedusia mwanadamu mara nyingi, Taenia saginata (Tegu wa Ng'ombe), ana urefu wa 20 m.

Kichwa cha tegu huitwa skoleksi (scolex) na kina kulabu na/au ogani za mfyonzo ili kujishikiza kwa ukuta wa utumbo. Mwili una pingili nyingi zinazozaliwa mfululizo mwishoni kwa skoleksi. Kila pingili ina ogani za jinsi na zile za mwisho, ambazo zina mayai yaliyoiva, zinaachwa na kutolewa kwa mwili pamoja na mavi. Kama mayai yakiliwa na mwenyeji wa kati lava wanatoa mayai na kukua. Baada ya muda fulani wanaingia kwa misuli na kuunda uvimbe (cyst). Mwenyeji wa kati akiliwa na mbuai lava wanakomaa katika utumbo.

Spishi zilizochaguliwa

hariri