Theodori wa Sykeon

Theodori wa Sykeon (Sykeon, Galatia, leo nchini Uturuki, karne ya 6 - 22 Aprili 613[1][2][3]) alikuwa tangu utotoni mkaapweke mwenye maisha magumu akawa maarufu kwa miujiza[4].

Picha takatifu ya Mt. Theodori.

Alipewa upadirisho akiwa na umri wa miaka 17 tu, akawa bila kupenda askofu wa Anastasiopoli[5] kwa miaka kumi hivi, ambapo alizidi kumuomba Patriarki wa Konstantinopoli amruhusu kurudi upwekeni, akamalizia maisha yake kama abati wa monasteri aliyoianzisha alipokuwa padri tu[6].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Aprili[7].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.