Theonas wa Aleksandria

Theonas wa Aleksandria alikuwa Patriarki wa mji huo wa Misri tangu mwaka 282 hadi kifo chake tarehe 10 Januari 300.

Theonas alikuwa msomi aliyevuta wengi kwenye Ukristo akajenga kanisa kwa heshima ya Mama wa Mungu.

Alimpinga na kumshinda kwa hoja Sabellius aliyefundisha kwamba Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ni nafsi moja tu.

Athanasi Mkuu alishuhudia kwamba tangu kale Theonas aliheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake au 28 Desemba[1][2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.