Thiago Rangel Cionek (alizaliwa Curitiba, Paraná, Brazil, 21 Aprili 1986) ni mchezaji wa soka ambaye anacheza kama beki wa kati wa klabu ya Italia S.P.A.L. na timu ya taifa ya Poland.

Thiago Cionek (2018)

Kazi ya klabu

hariri

Cionek alianza kazi yake na klabu ya Cuiabá Esporte Clube.

Alihamia Ulaya katika klabu ya GD Bragança iliyomo nchini Ureno kabla ya kurudi Brazili katika klabu ya Clube de Regatas Brasil.

Mwaka 2008, Cionek alirudi Ulaya, akicheza misimu minne na klabu ya Jagiellonia Białystok katika nchi ya Poland. Timu hiyo ilishinda Kombe la klabu za Poland la msimu wa 2009-10 na Poland SuperCup mwaka 2010.

Mnamo 11 Januari 2016, alijiunga na klabu yake ya tatu ya Italia iitwayo Città di Palermo ya Serie A.

  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Thiago Cionek kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.