Thomas Becket (Cheapside, London, Uingereza, 1118 (au 1120) – 29 Desemba 1170) alikuwa Askofu mkuu wa Canterbury tangu 1162 hadi kifodini chake kilichotokea wakati wa Misa katika kanisa kuu.

Mchoro mdogo katika kitabu cha Zaburi cha Uingereza, 1250 hivi, Walters Art Museum, Baltimore, Marekani.

Sababu ya kuuawa ni kubishana kwake na mfalme Henri II wa Uingereza juu ya haki na juu ya fadhili za Kanisa.

Kwa ajili hiyo alikuwa ameshafukuzwa kutoka jimbo lake na kutoka ufalme wote wa Uingereza.

Baada ya miaka sita aliweza kurudi nchini, lakini aliendelea kusumbuliwa sana hadi alipomuendea Kristo kwa kuchomwa na askari wa mfalme kwa upanga [1].

Muda mfupi baadaye Papa Alexander III alimtangaza mtakatifu mfiadini tarehe 21 Februari 1173. Ndivyo anavyoheshimiwa na Kanisa Katoliki na Anglikana.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Desemba[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • Barlow, Frank (1986). Thomas Becket. Berkeley, CA: University of California Press. ISBN 0-520-07175-1.
  • Barlow, Frank (2004). "Becket, Thomas (1120?–1170)". Oxford Dictionary of National Biography. Oxford University Press. doi:10.1093/ref:odnb/27201
     . http://www.oxforddnb.com/view/article/27201. Retrieved 17 April 2011.

Marejeo mengine

hariri
Maisha
  • Duggan, Anne (2005), Thomas Becket, London: Hodder Arnold.
  • Guy, John. Thomas Becket: Warrior, Priest, Rebel (Random House; 2012) 424 pages
  • Knowles, David (1970), Thomas Becket, London: Adam & Charles Black.
Historia
  • Duggan, Anne (1980), Thomas Becket: A Textual History of his Letters, Oxford: Clarendon Press.
  • Duggan, Anne (Hrsg.) (2000), The Correspondence of Thomas Becket, Archbishop of Canterbury (1162–1170). 2 Bände, lat./engl., Oxford: Clarendon Press.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.