Tigri na Eutropi (walifariki Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 404 hivi) walikuwa wafuasi wa askofu Yohane Krisostomo ambao, baada ya huyo kufukuzwa kutoka jimbo lake, waliuawa kwa kusingiziwa kwamba kwa hasira na kisasi walichoma kanisa na ofisi ya serikali[1]. [2]. Tigri alikuwa padri.

Tangu kale wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 12 Januari[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.