Tomboy ni neno la Kiingereza linalotumika kumaanisha ama kumuelezea msichana mwenye sifa za kiume. Neno hili linaweza kujumuisha kuvaa nguo zisizo za kawaida kwa msichana na kushiriki kikamilifu katika michezo au shughuli nyingine zinazohusishwa na wavulana.[1]

Neno "tomboy" limetokana na maneno mawili "tom" na "boy" yakimaanisha mvulana. Ingawa neno hili sasa linatumika kurejelea "wasichana wanaofanana na wavulana", asili yake inaonyesha kuwa maana yake imebadilika sana hadi kipindi hiki. [2]

Mwaka 1533, kulingana na kamusi ya Oxford ya Kiingereza, neno "tomboy" lilitumiwa kumaanisha "mvulana mkorofi, ama mvulana asiyekuwa na aibu".[3] Kufikia miaka ya 1570, hata hivyo, neno "tomboy" lilikuwa limechukua maana ya "mwanamke shupavu au asiye na adabu", hatimaye, mwishoni mwa miaka ya 1590 na mwanzoni mwa miaka ya 1600, neno hilo lilibadilika kuwa na maana yake ya sasa: "msichana ambaye ana tabia kama mvulana mkorofi”[3]"

Marejeo

hariri
  1. Who Are Tomboys and Why Should We Study Them?, SpringerLink, Archives of Sexual Behavior, Volume 31, Number 4
  2. King, Elizabeth (Jan 5, 2017). "A Short History of the Tomboy". Atlantic. Iliwekwa mnamo Nov 22, 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: url-status (link)
  3. 3.0 3.1 Abate, Michelle Ann (2015-06-04). "Tomboy". Keywords (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-12-13.
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tomboy kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.