Hagia Sophia

Hagia Sophia mjini Istanbul
Hagia Sophia kwa ndani
Mozaiki ya Yesu katika ukuta wa Hagia Sophia

Hagia Sophia ni jina la Kigiriki la kanisa kubwa mjini Istanbul - Konstantinopoli lililobadilishwa kuwa msikiti tangu 1453 na halafu kuwa makumbusho mwaka 1934. Jina linatokana katika Kigiriki Ἅγια Σοφία ("hekima takatifu") na kwa Kituruki inaitwa Ayasofya.

Ujenzi wa kanisa ulianzishwa mwaka 532 na Kaisari Justiniani I mtawala wa Roma ya Mashariki au Ufalme wa Byzanti. Alitaka kuwa na kanisa kubwa kuliko yote duniani akafaulu kwa sababu Hagia Sofia ilikuwa ukumbi mkubwa duniani hadi mwaka 1520. Jengo lilikamilishwa baada ya miaka mitano na Justiniani alipoingia mara ya kwanza aliita "Suleimani nimekushinda", akimfikiria mfalme Suleimani wa Israeli ya Kale aliyejenga hekalu la Yerusalemu.

Mwaka 1453 Waturuki Waislamu waliteka mji wa Konstantinopoli na kuifanya mji mkuu wa Dola la Osmani. Hapo Hagia Sofia likabadilishwa kuwa msikiti na Waturuki wakatamka jina la kigiriki kama "Ayasofya". Jengo la kanisa likaongezekwa minara minne ya mtindo wa Kiislamu.

Baada ya anguko la Waosmani katika vita kuu ya kwanza ya dunia kiongozi wa taifa Kemal Atatürk akaamuru jengo liwe makumbusho.

Viungo vya NjeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hagia Sophia kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.