Ukulele ni ala ya muziki yenye nyuzi nne ingawa nyuzi sita au nane pia huweza kutumiwa. Ala hii ilianzishwa karne ya 19 huko Hawaii na wahamiaji wa Kireno kutoka Madeira na Cabo Verde baada ya kuiga miundo ya magitaa madogo ya Kireno kama machete, cavaquinho, timple na rajão. Ukulele ilipata umaarufu huko Marekani katika karne ya 20 na baadaye umaarufu wake ukaenea dunia nzima.

Ukulele

Wahamiaji watatu ambao walikuwa ni watengeneza makabati, Manuel Nunes, José do Espírito Santo, na Augusto Dias wanaaminika kuwa ni watu wa kwanza kutengeneza ukulele.

Moja ya sababu zilizofanya ukulele kuwa ni moja ya ala muhimu kwenye muziki wa Kihawaii na utamaduni wake ilikuwa msaada mkubwa na uendelezaji wa ala hii uliofanywa na Mfalme Kalākaua.

Ukulele kawaida huwa na ukubwa wenye kuleta sauti za aina nne: soprano, concert, tenor na baritone.

Inasemekana kuna ubora wa ukulele kama ala ya muziki kwa watoto wanaopenda kujifunza na kucheza muziki. Ukelele ni ala ambayo imetengenezwa kwa nyuzi zinazotoa sauti mbalimbali. Ubora wake kwa watumiaji ni kuwa: si ya gharama, ni nyepesi kubeba, inatoa sauti nyororo, ni nzuri kwa watumiaji wanaoanza kujifunza na ni rahisi kutumia.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ukulele kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.