Cabo Verde

Jamhuri ya Cabo Verde (Kiswahili)
Repúblika di Kabu Verdi (Kikreole)
Bendera ya Cabo Verde Nembo ya Cabo Verde
(Bendera ya Cabo Verde) (Nembo ya Cabo Verde)
Lugha rasmi Kireno
Mji Mkuu Praia
Mji Mkubwa Praia
Serikali Jamhuri
Rais Carlos Veiga
Waziri Mkuu Ulisses Correia e Silva
Eneo km² 4,033
Idadi ya wakazi 543,767 (2018)
Wakazi kwa km² 123.7
Uchumi nominal Bilioni $2.042
Pesa Eskudo ya Cabo Verde
Kaulimbiu "Umoja, Kazi, Maendeleo"
Wimbo wa Taifa Chimbo ya Uhuru
Cabo Verde katika Afrika

Cabo Verde (ing. Cape Verde) ni nchi ya visiwa katika bahari ya Atlantiki mbele ya pwani ya Afrika ya Magharibi.

Ramani ya Cabo Verde

Umbali wake na Senegal ni km 460.

JiografiaEdit

Eneo la visiwa vyake kwa jumla ni km² 4,033.

Funguvisiwa vyake ina visiwa 15 katika vikundi viwili:

MijiEdit

Mji mkuu ni Praia katika kisiwa cha Santiago.

Miji mikubwa zaidi ni (takwimu za mwaka 2005): Praia (wakazi 113.364), Mindelo (wakazi 70.611), Santa Maria (wakazi 17.231), Pedra Badejo (wakazi 9.488) na São Filipe (wakazi 8.189).

HistoriaEdit

Hadi kufika kwa Wareno katika karne ya 15 visiwa vya Cabo Verde havikuwa na watu.

Wareno walianzisha mashamba ya miwa na kuleta watumwa kutoka bara la Afrika.

Cabo Verde ilikuwa pia kituo muhimu cha biashara ya watumwa kati ya Afrika na Amerika.

Wahamiaji kutoka Ulaya walikuwa pia Wahispania, Waitalia pamoja na Wayahudi na Waislamu waliokataliwa kukaa kwao Ureno.

WatuEdit

Kutokana na historia hiyo, leo idadi kubwa ya wakazi ni machotara waliozaliwa na Waafrika (waliochangia 56% ya DNA) na Wazungu (waliochangia 44%).

Lugha rasmi ni Kireno, lakini wakazi wanazungumza aina mbalimbali za Krioli iliyotokana na lugha hiyo.

Upande wa dini, walau 89.1% ya wakazi ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki (78.7%), lakini pia wa madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti (10.4%).

Kutokana na hali ngumu ya uchumi, wananchi wanaoishi nje ya Cabo Verde ni wengi kuliko wale wanaoishi nchini. Kati ya waliohama baada ya uhuru (1975), 500,000 wanaishi Marekani na 150,000 Ureno.

Tazama piaEdit

MarejeoEdit

     . http://www.earth.ox.ac.uk/~tony/watts/downloads/Pim_etal_2008.pdf. Retrieved 2015-07-18.
     . PMID 10100838
      . http://www.researchgate.net/publication/227504366_Emigration_return_and_development_in_Cape_Verde_the_impact_of_closing_borders.
     . https://www.geolsoc.org.uk/en/Publications/Supplementary%20Publications/2010/~/media/Files/GSL/shared/Sup_pubs/2010/18390SupPub.ashx.

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Cabo Verde kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.