Ukumbusho (liturujia)
Ukumbusho (kutoka kitenzi "kukumbuka"; kwa Kiyahudi זִכָּרוֹן, zikkaron; kwa Kigiriki ἀνάμνησις, anamnesis; kwa Kiingereza "memorial") ni neno zito katika teolojia na liturujia ya dini ya Uyahudi na Ukristo vilevile.
Ni tendo ambalo linataka kumfanya Mungu na watu kukumbuka tukio la historia ya wokovu. Tena, kwa wenye imani hiyo, si kama kukumbuka tukio lingine la zamana ambalo limepita tu. Ni kwamba kwa tendo hilo Mungu anafanya tukio liwepo upya kwa waliopo na kuwaletea neema zake ambazo zinawaelekeza kwenye utimilifu wa wokovu utakaopatikana baadaye.
Katika Uyahudi
haririNdivyo ilivyo hasa kwa Pasaka ya Kiyahudi iliyo ukumbusho wa Waisraeli kutolewa utumwani Misri kwa njia ya Musa (Kutoka 12,14).
Katika Ukristo
haririKanisa Katoliki linasadiki kuwa liturujia yote ni ukumbusho wa fumbo la wokovu ambalo Mungu Baba alilifanya kwa njia ya Yesu Kristo, kwa umwilisho, kifo na ufufuko wake.
Kwa namna ya pekee Ekaristi, iliyowekwa na Yesu mwenyewe katika karamu ya mwisho kama ukumbusho wake, inafanya fumbo hilo liwafikie waamini kwa neema zake.
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- [1] Archived 22 Aprili 2009 at the Wayback Machine. Zikkaron: Liturgical Remembrance and Sacred History
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |