Ursino wa Bourges (alifariki Bourges, leo nchini Ufaransa, karne ya 3) alikuwa askofu wa kwanza wa mji huo aliyemtangaza Kristo Bwana kwa umati.

Sanamu yake huko Villers-sur-le-Roule (Eure).

Kwa ajili ya waamini, wengi wao fukara, aligeuza nyumba ya Leokadi, seneta Mpagani wa Galia, kuwa kanisa [1].

Gregori wa Tours alisimulia habari zake kwa kuzichanganya na hadithi zisizoaminika kihistoria[2].

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 9 Novemba[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.