Ushiriki wa Kiraia

ushiriki wa wananchi katika serikali

Ushiriki wa kiraia ni kitendo kinachohusisha mtu binafsi au kikundi cha watu katika kushughulikia mambo yanayohusu jamii. Ushiriki wa kiraia unahusisha jamii zinazofanya kazi kwa pamoja au mtu binafsi anaefanya shughuli za kisiasa na zisizo za kisiasa kwa lengo la kulinda maadili  ya umma au kuleta mabadiliko katika jamii.Lengo la ushiriki wa kiraia ni kuwasilisha matakwa ya jamii nakulinda usawa katika jamii.[1]

Kujitolea ni aina muhimu ya ushiriki wa raia. Pichani ni watu wa kujitolea wakifanya usafi baada ya Kimbunga Sandy cha 2012.

Ushiriki wa kiraia ni kitendo kinachohusisha watu kufanya kazi kwa pamoja ili kulinda matakwa au mahitaji ya jamii "kazi kwa ajili ya demokrasia " (Checkoway & Aldana, 2012). Chini ya uwakilishi wa vikundi vya watu wachache, watu wenye kipato cha chini na vikundi vya vijana. Kwa upande mwingine, masuala yenye vikundi vya watu wenye ushawishi mkubwa yanawasilishwa kwa haraka ili kutatua matatizo yanayoikumba jamii hiyo.(Griffin & Newman, 2008). [2]

Faida na changamoto hariri

Ushiriki wa kiraia kwa ujumla unakuza ushirikishwaji wa jamii na serikali  kutokana na  (ICMA: Leaders at the Core of Better Communities.). Umuhimu wa ushiriki wa kiraia ni kama ifuatavyo

• Kufikia maamuzi yasiyo nje na sheria

• Inajenga uaminifu kati ya wananchi na serikali ambayo inasaidia kujenga tabia katika mikutano ya hadhara

• Kufikia malengo yenye matokeo chanya kwenye masuala magumu pia inasaidia viongozi waliochaguliwa na wananchi kutatua matatizo mbalimbali

• Inakuza mawazo na kupata suluhu

• Inatengeneza wananchi wanaojituma na kupunguza wahitaji katika jamii

• Inafanya kazi kuwa rahisi

Kwenye faida za ushiriki wa kiraia kuna changamoto zake. Changamoto zinatokana na  sababu tofauti kutokana na (ICMA) kama ukosefu wa uaminifu,ufafanuzi wa majukumu na mda wa kuyafanya majukumu husika.

• Ushiriki wa kiraia unachukua mda kuonyesha mabadiliko chanya kuliko serikali ikifanya yenyewe moja kwa moja.

• Ushiriki wa kiraia ili ufanikiwe lazima kuwe na uwazi na uaminifu unahitajika kati wananchi na serikali.

Mchango wa jamii hariri

Ushirikiano wa jamii unahusisha nafasi za kidemokrasia ambapo watu wako tayari kujadili masuala mahususi kuhusu maslahi ya jamii na mbinu za kufanya mabadiliko yanayohitajika.Wananchi wanaweza kupata taarifa kuhusu mabadiliko yajayo, suluhu zinazopendekezwa kwa matatizo yaliyopo, n.k. Vyuo vikuu vinatoa fursa zaidi na kutarajia wanafunzi zaidi kushiriki katika kazi ya kujitolea katika jamii. [3]

Teknolojia hariri

Matumizi ya Televisheni hariri

Putman aliangalia kwanini mtaji wa kijamii umekuwa ukipungua kwenye mojawapo ya maeneo ambayo utafiti huo ulifanywa na televisheni na kuona athari zake katika shughuli za kijamii na kiraia. Shah anaandika kwamba Putnam alipata kadiri televisheni mtu anavyotazama, ndivyo anavyokuwa hai katika shughuli za nje. Hii inaonyeshwa na kuongezeka kwa televisheni  mnamo mwaka 1960 ushirikiano wa kiraia. Waligundua kwamba ingawa habari na programu za elimu zinaweza kusaidia maarifa ya kiraia, lakini ukosefu wa kujihusisha na shughuli za nje na matukio ya kijamii huumiza ushiriki.

Marejeo hariri

  1. "ushiriki wa kiraia". www.apa.org. 
  2. Checkoway, B., & Aldana, A. (2013). Four forms of youth civic engagement for diverse democracy. Children and Youth Services Review, 35(11), 1894–1899. doi:10.1016/j.childyouth.2013.09.005
  3. Ekman, Joakim; Amnå, Erik (June 2012). "Political participation and civic engagement: towards a new typology". Human Affairs 22 (3): 283–300. doi:10.2478/s13374-012-0024-1.  Unknown parameter |doi-access= ignored (help); Check date values in: |date= (help)