Programu tumizi, maarufu kama Protu (kwa Kiingereza: App), ni programu za tarakilishi zinazotumiwa hasa na simujanja na saajanja na ni tofauti na zile zinazotumiwa na tarakilishi.

Mwaka 2009, mwandishi wa makala za teknolojia David Pogue alisema kuwa simujanja mpya zitapewa jina la utani "app phones" ili kuzitofautisha na simu zilizotangulia.[1].

Neno "app", ambalo ni kifupi cha "software application", limekuwa maarufu toka wakati huo. Mwaka 2010 neno hili liliteuliwa na American Dialect Society kuwa "Neno la Mwaka".[2]

Programu hizi zina manufaa makubwa kwa watumiaji wa simujanja kwa masuala kama ya muziki, video, michezo kama vile pokeman[3], vitabu, habari, afya, biashara, n.k. Hata hivyo, protu hutumika visivyo pia kwa masuala kama vile wizi wa taarifa za siri, wizi wa nywila na udukuzi.[4]

Mbinu za kubuni usanifu wa maombi ya mtandao hutumiwa. Programu ya wavuti ina sehemu za mteja na seva, na hivyo kutekeleza teknolojia ya "mteja-seva". Sehemu ya mteja inatekeleza kiolesura cha mtumiaji, huunda maombi kwa seva na kuchakata majibu kutoka kwayo.

Marejeo

hariri
  1. Pogue, David. "A Place to Put Your Apps", New York Times, November 4, 2009. Retrieved on January 22, 2013. 
  2. ""App" voted 2010 word of the year by the American Dialect Society (UPDATED) American Dialect Society". Americandialect.org. 2011-01-08. Iliwekwa mnamo 2012-01-28.
  3. Jackson, Anthony A. (2018-11-01), "Pokemon Jupiter Rom – The Full Story", Original Console Games (kwa American English), ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-14, iliwekwa mnamo 2018-11-29 {{citation}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  4. "Wifi Hacker app". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-23. Iliwekwa mnamo 2018-08-17.
  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.