VP Records ni jina la studio ya kurekodi muziki wa Reggae inayojisimamia ambayo inapatikana mjini Queens, New York. Inajulikana sana kwa kuwatayarishia muziki waimbaji wengi wa Kikaribi.

VP Records
Imeanzishwa 1979
Mwanzilishi Vincent "Randy" Chin
Patricia Chin
Nchi United States
Mahala Queens, New York
Tovuti Official website

VP Records ni lebo iliyoanzishwa mnamo 1979 na marehemu Vincent "Randy" Chin na mkewe Patricia Chin, Wajamaica wenye asili ya Kichina ambao walikuwa wakimiliki lebo ya Randy's Records Mjini Kingston, Jamaica (inavyoonekana katika filamu ya ‘’Rockers’’) na pia Studio 17. Katika ti ya miaka ya 1970s wawili hawa walihamia Jiji la New york, huku wakianzisha duka la kuuza rekodi mjini Brooklyn liitwalo VP Records mnamo 1975, mahali ambapo waliuza na kusambaza rekodi kutoka huko. Mnamo 1979 walihamisha makao ya gala hilo la muziki kwenda Queens, Jamaica. Mnamo 1993, lebo ya rekodi ilianzishwa baada ya duka la rekodi kunawili. Jina la lebo limetokana na nukta za kwanza za majina ya waanzilishi.

Muziki

hariri

Lebo hii ilijiimarisha kuwa moja kati ya lebo huru kubwa zaidi kwa muzikiwa mienendo ya Reggae na dancehall. Kwa umaarufu wa sauti ya riddim kutoka mapema mwaka wa 2000, lebo hii ilileta ufanisi mkuu kwa wasanii wengi katika dunia nzima kama vile Sean Paul kupitia kwa mikataba ya lebo na lebo ya Virgin Music Canada na Atlantic Records inayomilikiwa na Warner Music. Lebo hii maranyingi huhusishwa na umaarufu mkubwa wa Elephant Man ambaye pia anajilikana kama ‘’Energy God’’ au ‘’Ele’’ kupitia kazi yake na Bad Boy Records. Nembo ya VP Records ni “Maili mbele katika muziki wa Reggae”. Kando na reggae, VP pia inajulikana kwa mwenendo wa dancehall na Soca. VP pia ilitoa mshururu wa albamu ambazo zinajikitha katika sauti za ‘’Riddims’’, ambazo zinashirikisha wasanii mbalimbali.

VP imewahi kushindatuzo la Billboard kama lebo huru bora zaidi (Best Independent Label) kwa miaka miwili ma pia imepokea tuzo la Lebo bora zaidi ya Reggae kwa miaka mitatu mtawalia. Pia ilifuzu kwa tuzo la ‘’Best Independent Reggae Label’’ la 2003 la Billboard Hip-Hop and R&B, na pia ilikuwa imetajwa na kushirikishwa katika machapisho kama Vibe magazine, New York Times, Los Angeles Times, Billboard, na Time magazine.

Lebo hiyo sasa inasimamiwa na wana wa Bw.Chin, Randy na Christopher huku Bi Patrici Chin akiendelea kutoa usaidizi wa kuendelea kuitunza kampuni hii ya marehemu mumewe.

Wengi wa wasanii wa lebo hii wamehusika katika utata kutokana na maneno ya nyimbo zao ambayo huchochea vurugu (ukiwemo uuaji) dhidi wale wanaojihusisha kimapenzi kati ya jinsia moja.

Wasanii

hariri

Wasanii wa awali

hariri

Viungo vya Nje

hariri