Waberiberi
Waberiberi ni wakazi asilia wa Afrika ya Kaskazini kuanzia Moroko hadi Misri na nchi za Sahara. Wenyewe wanajiita Amazigh (au: Imazighen) yaani "watu huru".
Kabila lao mojawapo linalojulikana hasa ni Watuareg wanaokalia maeneo ya jangwa kubwa la Sahara.
Leo hii wamepungua kwa sababu wengi wamezoea kutumia lugha ya Kiarabu, hivyo wanahesabiwa kati ya Waarabu.
Wanaoendelea kutumia lugha ya Kiberiberi kama lugha ya kwanza ni:
- takriban theluthi ya watu huko Moroko,
- asilimia 10-15 nchini Algeria,
- labda asilimia 3 nchini Libya,
- idadi ndogo zaidi wako Tunisia,
- laki kadhaa huishi katika nchi za Sahara kama Mali na Niger halafu
- wako kwa idadi ndogo Burkina Faso, Misri na Mauritania.
- Kutokana na uhamiaji kuna nusu milioni nchini Ufaransa.
Katika nchi kavu jangwani au karibu na jangwa maisha yao ni ya ufugaji na kuhamahama. Mlimani wanalima. Leo hii ni hasa Watuareg wanaoendelea na maisha ya kuhamahama.
Historia
haririKatika historia wamejulikana tangu ilipoanza kuandikwa. Waroma na Wagiriki wa Kale waliwaita kwa majina kama Wanumidia, Wagaramanti au Walibya.
Kabla ya unenezaji wa Uislamu wengi walikuwa Wakristo na mashuhuri kati hao alikuwa Monika, mama wa Agostino wa Hippo.
Mberiberi anayejulikana sana leo ni mchezaji wa mpira wa Ufaransa Zinédine Zidane.
Viungo vya nje
hariri- Richard L. Smith, Ferrum College, What Happened to the Ancient Libyans? Chasing Sources across the Sahara from Herodotus to Ibn Khaldun, Journal of World History, vol. 14, no. 4, 2003 Online article
- Amazigh Startkabel Ilihifadhiwa 11 Julai 2005 kwenye Wayback Machine..
- Institut Royal de la Culture Amazighe.
- The New Mass Media and the Shaping of Amazigh Identity.
- Number Systems and Calendars of the Berber Populations of Grand Canary and Tenerife.
- Encyclopedia of the Orient -- Berbers .
- Flags of the World -- Berbers/Imazighen Ilihifadhiwa 4 Agosti 2006 kwenye Wayback Machine..
- www.mondeberbère.com Ilihifadhiwa 16 Machi 2012 kwenye Wayback Machine..
- CMA: Congrès Mondial Amazigh Ilihifadhiwa 21 Machi 2016 kwenye Wayback Machine..
- Photo Gallery of Berbers and Touregs from Erg Chebbi area of Moroccan Sahara Ilihifadhiwa 22 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine.