Wadi Draa (pia: "Oued Dra") ni mto mrefu wa Moroko. Unaanza katikati ya nchi kwenye milima ya Atlasi yanapoungana matawimto ya Dadès and Imini.

Draa (Wadi Draa)
Bonde la Draa
Chanzo Maungano ya matawimito ya Dades na Imini katika milima ya Atlas
Nchi Moroko, Aljeria
Urefu 1,100 km
Kimo cha chanzo ?
Mkondo ?
Eneo la beseni 29,500

Mwanzoni unaelekea kusini mashariki hadi Tagunit halafu kusini-magharibi ukifuata mpaka wa Algeria na Moroko hadi mdomo wake kwenye bahari ya Atlantiki.

Ni mara kwa mara tu ya kwamba maji yake yanafika baharini, wakati mwingi inakauka njiani.

Miji muhimu mtoni ni Warzazate (Ouarzazate) na Zagora.

Tazama pia

  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wadi Draa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.