Wafiadini wa Mlango wa Shaba

Wafiadini wa Mlango wa Shaba (walifariki Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 730 hivi) walikuwa Wakristo waliouawa na kaisari Leo III wa Bizanti kwa sababu ya kuheshimu picha takatifu na kutaka kuzuia isivunjwe ile ya Mwokozi kwenye Mlango wa Shaba[1].

Walikuwa wengi, lakini kati yao wanatajwa kwa jina Juliani, Machani, Yohane, Yakobo, Alesi, Demetri, Fosyo, Petro, Leonsi, Maria na Gregori tu[2] [3].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 9 Agosti[4].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.