Wafiadini wa Ponto

Wafiadini wa Ponto (walifariki 300 hivi) ni kundi kubwa la Wakristo wa Ponto, leo nchini Uturuki) ambao waliuawa kikatili sana wakati wa dhuluma ya kaisari Masimiano kwa sababu ya imani yao[1]. Baadhi walimwagiwa risasi ya moto, baadhi waliteswa kwa kuingiziwa makuchani matete yaliyochangwa na kwa namna nyingine mbalimbali za kurudiwakurudiwa.

Tangu kale wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao inaadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Februari[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.