Wafiadini watano wa Turo
Wafiadini watano wa Turo (walifariki Turo, Finisia, leo nchini Lebanoni, 300 hivi) walikuwa vijana wa mji huo waliouawa kwa ajili ya imani ya Kikristo katika dhuluma ya kaisari Dioklesyano.
Baada ya kuteswa kikatili kwa mijeledi katika mwili mzima, walitupwa uchi katika uwanja wa michezo kama chakula kwa wanyama mbalimbali lakini wakaonyesha msimamo imara kabisa. Mmojawao, asiyefikia miaka 20 na asiyefungwa na minyororo, alinyosha mikono kama msalabani kumuomba Mungu. Baada ya wanyama hao kutowashambulia, walichomwa kwa upanga[1].
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 20 Februari[2].
Tazama pia
haririTanbihi
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |