Walowezi (kutoka kitenzi "kulowea"; pia: setla, kutoka Kiingereza "settler") ni watu ambao wamehamia katika eneo fulani na kuanzisha makazi ya kudumu pale, hata mara nyingi kulitwaa eneo hilo. Makazi mara nyingi hujengwa kwenye ardhi ambayo inadaiwa au inayomilikiwa na watu wengine.

Picha inayoonyesha walowezi wa kwanza wa Karne za kati wakifika Aisilandi.

Wao wenyewe wakati mwingine huondoka katika kujitafutia riziki au uhuru wa dini[1].

Mara nyingine walowezi huungwa mkono na serikali au nchi kubwa au tajiri[2].

Sababu za uhamiaji

hariri

Sababu za kuhama kwa walowezi hutofautiana, lakini mara nyingi huwa ni mambo yafuatayo: hamu ya mwanzo mpya na maisha bora katika nchi ya kigeni, hali duni ya kifedha, dhuluma ya kidini[1], ya kijamii, ya kiutamaduni au ya kikabila[2], kukandamizwa kisiasa, na sera kutoka serikali zinazowapa motisha wananchi kwa lengo la kuhamasisha makazi ya kigeni.[3]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 "Mormon Settlement". historytogo.utah.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-03-17. Iliwekwa mnamo 2018-08-04.
  2. 2.0 2.1 "Financial Interests Back Settlement of Jews in Kenya | Jewish Telegraphic Agency". www.jta.org (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2018-08-04.
  3. Wolfe, Patrick (2006-12). "Settler colonialism and the elimination of the native". Journal of Genocide Research (kwa Kiingereza). 8 (4): 387–409. doi:10.1080/14623520601056240. ISSN 1462-3528. {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help)
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Walowezi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.