Uhamiaji wa binadamu

Uhamiaji wa binadamu ni mchakato wa watu kutoka sehemu moja kwenda hadi nyingine kwa nia ya kuanzisha makazi ya kudumu au ya muda katika eneo jipya. Kwa kawaida, watu husafiri masafa marefu, ndani mwa nchi au kutoka nchi moja hadi nyingine.

Kiwango cha uhamiaji duniani.

Watu wanaweza kuhama kama watu binafsi, kama familia au katika makundi makubwa.[1]

Mtu anayetoroka maafa ya asilia au vita vya wenyewe kwa wenyewe huitwa mkimbizi au mkimbizi wa ndani kama anahamia ndani mwa nchi. Pia, kuna watu ambao hutafuta kimbilio kutokana na kuteswa kwa ajili ya msimamo wa siasa au dini.

Wahamahamaji hawachukuliwi kuwa wahamiaji kwa kuwa hawana nia ya kufanya makazi na kuhama kwao ni kwa msimu tu. Pia, shughuli za watu kusafiri kwa madhumuni ya utalii, upelelezi au hija si uhamiaji.

Takwimu za uhamiaji

hariri
 
Sehemu ya wahamiaji katika kila nchi ya ulimwengu katika mwaka 2015.[2]

Makadirio kadhaa ya takwimu za uhamiaji katika dunia yapo.

Maendeleo ya hivi karibuni katika utafiti wa uhamiaji kupitia mtandao unawezesha kuelewa vizuri zaidi mwelekeo wa uhamiaji na nia za uhamiaji.[5][6]

Kiwango kikubwa cha uhamiaji hufanyika katika nchi za kaskazini na nchi za kusini. Wahamiaji wengi kutoka nchi zilizoendelea huhama kuenda nchi zilizoendelea zaidi na takriban 43% ya wahamiaji kutoka nchi zinazoendelea huhama kuenda nchi zingine zinazoendelea.

Mfuko wa Umoja wa Mataifa kuhusu Idadi ya Watu ilitoa ripoti kwamba nchi za kaskazini zilipata ongezeko kubwa zaidi la wahamiaji tangu mwaka 2000 (milioni 32) ikilinganishwa na nchi za Kusini (milioni 25), nchi za kusini zilipata ukuaji wa kiwango kikubwa zaidi. Kati ya mwaka 2000 na mwaka 2013 wastani wa kiwango cha mabadiliko ya idadi ya wahamiaji katika nchi zilizoendelea (2.3%) ilizidi kidogo ile ya nchi zinazoendelea (2.1%).

Marejeo

hariri
  1. "Migrations country wise". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-02-11. Iliwekwa mnamo 7 Juni 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link). One of the major migration rushes took place in the gold run in 19th century in California, Australia, and Africa.
  2. Kigezo:WebbrefSV
  3. http://siteresources.worldbank.org/INTLAC/Resources/Factbook2011-Ebook.pdf
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-04-21. Iliwekwa mnamo 2018-08-04.
  5. Oiarzabal, P. J.; Reips, U.-D. (2012). "Migration and diaspora in the age of information and communication technologies". Journal of Ethnic and Migration Studies. 38 (9): 1333–1338. doi:10.1080/1369183X.2012.698202.
  6. Reips, U.-D., & Buffardi, L. (2012). Studying migrants with the help of the Internet: Methods from psychology, Journal of Ethnic and Migration Studies, 38(9), 1405–1424. doi:10.1080/1369183X.2012.698208 http://www.uni-konstanz.de/iscience/reips/pubs/papers/2012ReipsBuffardi_JEMS.pdf