Wanna Be Startin' Somethin'

"Wanna Be Startin' Somethin'" ni wimbo wa mwanamuziki wa R&B-pop wa Kimarekani, Michael Jackson. Wimbo unatoka katika albamu yake ya sita akiwa kama msanii wa kujitegemea ya mwaka wa 1982, Thriller. Wimbo ulitolewa ukiwa kama single ya nne kutoka kwenye albamu hiyo mnamo tar. 8 Mei 1983, na kushika nafasi ya tano kwenye chati za Billboard Hot 100 singles, kwenye chati za Marekani - Hot Black Singles na Hot Dance Club Songs na chati za UK Singles Chart kote ilishika nafasi ya nane. Wimbo huu wa "Wanna Be Startin' Somethin'" aliurekodi upya akiwa na msanii wa hip hop Akon kwa ajili ya toleo jipya la 2008 la albamu ya Thriller 25 ikiwa chini ya jina la "Wanna Be Startin' Somethin' 2008" na kutolewa kama single nchini Marekani na kushika nafasi ya 48 kwa Marekani peke yake.

“Wanna Be Startin' Somethin'”
“Wanna Be Startin' Somethin'” cover
Single ya Michael Jackson
kutoka katika albamu ya Thriller
Imetolewa 8 Mei 1983
Muundo 7" vinyl
Imerekodiwa 14 Aprili–8 Novemba 1982 kwenye studio ya Westlake Recording Studios, Los Angeles, California
Aina R&B, funk, pop, soul
Urefu 6:02 (toleo la albamu)
4:17 (toleo la single)
Studio Epic
Mtunzi Michael Jackson
Mtayarishaji Quincy Jones, Michael Jackson
Mwenendo wa single za Michael Jackson
"Beat It"
(1983)
"Wanna Be Startin' Somethin'"
(1983)
"Human Nature"
(1983)

Wimbo wa Kiafrika

hariri

Wimbo unaishia ukiwa na kiitikio kinachorudia-rudia kuimba "Mama-se, mama-sa, ma-ma-coo-sa". Kwa mujibu wa mwandishi Mark Anthony Neal, "mashairi ya wimbo huu yalichukuliwa moja kwa moja kutoka kwa mwanamuziki na mpiga talumbeta wa Kikamerun Manu Dibango ambaye alivunja rekodi kwenye soko la muziki huko Amerika mnamo 1973 na kibao chake cha 'Soul Makossa'." Kelef Sanneh wa gazeti la The New Yorker, alieleza kwamba "Soul Makossa", "kilikuwa kibao [kikali], katika Afrika, Ulaya, na huko Amerika, ambamo ilionekana kama kibao cha kwanza cha aina ya disco". Pia, Sanneh alieleza kwamba, "[Dibango] aliuita wimbo wake makossa kwa kufuatia dansi ya Kikamerun, lakini yeye alinyoosha neno litokalo, [na] kusikika [inacheza kama]: 'Ma-mako, ma-ma-ssa, mako-makossa'."[1] Japokuwa wimbo wa Jackson unatofautisha maneno ya Dibango, toleo la Jackson linakosea kutaja maneno yale anayoyasema Dibango wimboni mwake.

Orodha ya nyimbo

hariri
Toleo la Marekani
  1. "Wanna Be Startin' Somethin'" (7" liohaririwa) – 4:17
  2. "Wanna Be Startin' Somethin'" (biti) – 6:30
Toleo la Uingereza
  1. "Wanna Be Startin' Somethin'" (album version) – 6:02
  2. "Rock with You" (laivu akiwa na The Jacksons) – 3:58

Mamixi yake

hariri
  1. Toleo la Albamu – 6:03
  2. 12" version – 6:30
  3. Biti – 6:30
  4. 7" liohaririwa – 4:17
  5. Brothers in Rhythm House Mix – 7:40
  6. Tommy D's Main Mix – 7:35
  7. "Wanna Be Startin' Somethin' 2008" (akiwa na Akon) - 3:45
  8. "Wanna Be Startin' Somethin' 2008" (akiwa na Akon) (Johnny Vicious Radio Mix) - 3:36
  9. "Wanna Be Startin' Somethin' 2008" (akiwa na Akon) (Johnny Vicious Club Remix) - 9:03
  10. "Wanna Be Startin' Somethin' 2008" (akiwa na Akon) (Johnny Vicious Warehouse Thrilla Dub) - 7:23
Chati (1983) Nafasi
iliyoshika
Australian Singles Chart 25
Dutch Top 40[2] 1
UK Singles Chart[3] 8
U.S. Billboard Hot 100 5
U.S. Billboard Hot Black Singles 1
Chart (2008) Peak
position
Australian Singles Chart[4] 8
Belgian Singles Chart[5] 15
Canadian Hot 100[6] 32
Czech Republic Singles Chart[7] 50
Danish Singles Chart[8] 29
European Hot 100 Singles[9] 87
French Singles Chart[10] 10
German Singles Chart[11] 63
Greek Singles Chart[12] 10
Italian Singles Chart[5] 20
Japan Hot 100[13] 52
Luxembourg Singles Chart[14] 23
Macedonian Radio Chart[15] 4
New Zealand Singles Chart[16] 4
Swedish Singles Chart[17] 3
Swiss Singles Chart[18] 30
UK Singles Chart[19] 69
U.S. Billboard Hot 100[20] 81
U.S. Billboard Pop 100[20] 48
Chati (2009) Nafasi
iliyoshika
UK Singles Chart 57
U.S. Billboard Hot Digital Songs[21] 20
  • 1983: Michael Jackson
  • 2008: Michael Jackson with Akon
  • 2009: Michael Jackson

Matunukio

hariri
Toleo Nchi Matunukio Mauzo
2008 Australia Dhahabu[22] 35,000+

Chati za Mwishoni mwa Mwaka

hariri
Mwaka Nchi Chati Ngazi
2008 Australia ARIA #65[23]

Vyanzo

hariri

Marejeo

hariri
  1. Sanneh, Kelef. "Michael Jackson." The New Yorker, 9 Julai 2009. [1]
  2. "De Nederlandse Top 40, week 30, 1983". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-03-20. Iliwekwa mnamo 2008-02-23.
  3. h8p://www.everyhit.com
  4. Australian ARIA Top 50 Singles Chart. ARIA Charts. Retrieved on 4 Februari 2008.
  5. 5.0 5.1 ultratop.be - Michael Jackson with Akon - Wanna Be Startin' Somethin' 2008
  6. "Billboard.com - Charts - Singles - Canadian Hot 100". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-01-14. Iliwekwa mnamo 2009-07-16.
  7. Čns Ifpi
  8. Denmark singles chart
  9. Europe singles chart
  10. France singles
  11. germany
  12. "Ελληνικό Chart". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2003-06-05. Iliwekwa mnamo 2009-07-16.
  13. Japan Singles Chart
  14. ELDORADIO, LUXEMBOURG'S HITRADIO – 105.0 & 107.2 MHz FM - Music / Chartbreaker
  15. "Antenna5". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-21. Iliwekwa mnamo 2009-07-16.
  16. nztop40.com
  17. "The Michael Jackson Fan Club - Charts Update Sweden". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-07. Iliwekwa mnamo 2009-07-16.
  18. Swiss singles chart
  19. "Chart Stats : UK Singles Chart". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-03-03. Iliwekwa mnamo 2008-03-03.
  20. 20.0 20.1 "Billboard.com - Artist Chart History - Michael Jackson". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-02-02. Iliwekwa mnamo 2008-02-02.
  21. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-04. Iliwekwa mnamo 2009-07-16.
  22. http://aria.com.au/pages/httpwww.aria.com.aupageshttpwww.aria.com.aupagesARIACharts-Accreditations-2008Singles.htm
  23. http://www.aria.com.au/pages/aria-charts-end-of-year-charts-top-100-singles-2008.htm

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wanna Be Startin' Somethin' kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.