Thriller ni albamu ya sita kutoka kwa msanii wa rekodi wa Kimarekani Michael Jackson. Albamu ilitolewa mnamo tar. 30 Novemba 1982 katika studio ya Epic Records. Hili toleo la pili la albamu lililopata mafanikio makubwa baada ya ile ya mwaka 1979, Off the Wall. Thriller imefanywa aina sawa na ile ya Off the Wall, ikiwemo funk, disco, soul, soft rock, R&B na pop. Hata hivyo, mashairi ya Thriller' yanadili sana na mambo ya giza, ikiwemo na vitisho na uchawi.

Thriller
Thriller Cover
Studio album ya Michael Jackson
Imetolewa 30 Novemba 1982
Imerekodiwa 14 Aprili – 8 Novemba 1982
Westlake Recording Studios
(Los Angeles, California)
Aina R&B, pop, rock
Urefu 42:19
Lebo Epic
EK-38112
Mtayarishaji Michael Jackson
Quincy Jones
Tahakiki za kitaalamu
Wendo wa albamu za Michael Jackson
Off the Wall
(1979)
Thriller
(1982)
Bad
(1987)
Single za kutoka katika albamu ya Thriller
  1. "The Girl Is Mine"
    Imetolewa: 18 Oktoba 1982
  2. "Billie Jean"
    Imetolewa: 3 Januari 1983
  3. "Beat It"
    Imetolewa: 14 Februari 1983
  4. "Wanna Be Startin' Somethin'"
    Imetolewa: 8 Mei 1983
  5. "Human Nature"
    Imetolewa: 3 Julai 1983
  6. "P.Y.T. (Pretty Young Thing)"
    Imetolewa: 19 Septemba 1983
  7. "Thriller"
    Imetolewa: 23 Januar, 1984
Toleo Maalumu la 2001
Toleo Maalumu la 2001


Albamu ulitumia bajeti ya matayarisho yake kwa Dola ya US$750,000. Kazi ya kurekodi ilichukua nafasi kati ya Aprili na Novemba 1982 kwenye studio ya Westlake Recording Studios ya mjini Los Angeles, California. Albamu ilisaidiwa na mtayarishaji Quincy Jones, Jackson ametunga nyimbo nne katika nyimbo tisa za albamu ya Thriller'. Kwa kufuatia kutolewa kwa single ya kwanza kutoka katika albamu, "The Girl Is Mine", kukawa na baadhi ya watafiti waliofikiria kwamba albamu ya Thriller itakuwa na rekodi ndogo.

Kwa kufuatia kutolewa kwa single ya pili ya "Billie Jean", albamu ikapata chati katika nchi kibao duniani. Katika nafasi ilizoshika, albamu ikauza nakala milioni kadhaa katika wiki. Baada ya mwaka kwisha, Thriller ikawa—na hadi sasa imebaki—kuwa albamu-yenye-mauzo-bora kwa muda wote. Mauzo yake yalikadiriwa kuuzwa nakala kati ya milioni 47–109 kwa mauzo ya dunia nzima.

Nyimbo saba kutoka albamu zilitolewa kama single, na zote zilifikia katika 10 kumi bora za Billboard Hot 100. Albamu imevunja rekodi ya tuzo nane za Grammy Awards katika ugawaji wa tuzo hizo za 1984 Grammys, ikiwa sambamba kabisa na ushindi wa aina tofauti, yaani, muziki wa—pop, R&B na rock.

Thriller imepelekea kumpa Jackson hadhi ya kuwa nyota mkali wa pop wa karne ya 20, na kumwezesha kuuvunja ukuta wa ubaguzi wa rangi kwa kupitia kuonekana kwake kwenye MTV na kukutana na Rais Ronald Reagan katika ikulu ya Marekani, White House. Albamu hii ni moja kati ya albamu zilizotumia muziki wa video kupata mafanikio makubwa kabisa ya promosheni—video hizo ni pamoja na "Thriller", "Billie Jean" na "Beat It" ambazo zote zilipata mzunguko wa kawaida kwenye MTV.

Mnamo mwaka wa 2001, toleo maalumu la albamu lilitolewa, ambalo limejumlisha baadhi ya mahojiano ndani yake, demo rekodi na wimbo wa "Someone In the Dark", ambao ulijishindia tuzo-Grammy kutoka katika hadithi ya kitabu cha E.T. the Extra-Terrestrial.[3] Mnamo mwaka wa 2008, albamu ilitolewa tena upya ikiwa kama Thriller 25, ikiwa imeambatana na re-mix za nyimbo kadhaa ambazo zimeshirikisha wasanii kadhaa wa R&B, baadhi ya nyimbo ambazo awali hazikutolewa na DVD.

Thriller imepata namba 20 kwenye gazeti la Rolling Stone 500 Albamu Bora ya Muda ya Karne mnamo 2003, na ikaorodheswa na National Association of Recording Merchandisers ikiwa nafasi ya tatu ya albamu Albamu Kali 200 za Karne.

Historia

hariri

Albamu iliyopita ya Jackson Off the Wall (1979) ilipata mafanikio makubwa na kupewa nyota kadhaa katika ripoti ya mafanikio yake.[4][5] Pia ilipata mafanikio makubwa sana kibiashara, na ikatokea kuuza nakala zaidi ya milioni 20 duniani kote.[6] Miaka kati ya Off the Wall na Thriller kilikuwa kipindi cha mpito cha mwimbaji huyu, ulikuwa muda wa kuongeza uhuru na kuiangaikia familia yake. Pale Jackson alivyofikisha umri wa miaka 21 mnamo mwezi wa Agosti 1979, akamtimua baba yake kazini, Joseph Jackson kuwa kama meneja wake na kumweka Bw. John Branca.[7]

Baada ya kumtimua mzee wake, Jackson akamwakikishia Branca kwamba anataka kuwa "nyota mkubwa katika biashara ya maonyesho" na "tajiri mkubwa". Michael alijisikia unyonge kuhusu kile alichokipata katika uchakalikaji wa chini wa albamu yake ya Off the Wall, alieleza, "Ilikuwa sio vizuri kabisa yaani albamu haikupata hata tuzo ya Grammy ya Rekodi Bora ya Mwaka na haitotokea tena.

Pia akajisikia anathamani kabisa katika soko la muziki; mnamo mwaka wa 1980 pale Jackson alipomwomba mchapishaji wa Rolling Stone endapo watapenda kusanifisha kasha ya hadithi inayomuhusu yeye, mchapishaji akakataa, ambamo Jackson alijibu na kusema kwamba, "Nilishaambiwa tena na tena kwamba watu weusi katika kava la magazeti hawauzi nakala kabisaa ... Ngoja kwanza. Ipo siku hayo magazeti yatakuja kuniomba kwa ajili ya mahojiano. Labda nitawapatia jibu moja. Na labda nisiwapatie."[8]

Mnamo mwaka wa 1973, baba wa Jackson ameanzisha mahusiano ya kimapenzi ya siri na mwanamke mwenye umri wa miaka 20 kiumri ni mdogo kuliko yeye; wawili hao wakapata mtoto kisiri. Mnamo mwaka wa 1980, Joseph Jackson akawaelezea familia yake kuhusu mahusiano yake na mtoto aliyemzaa. Jackson, akawa keshakasirishwa na baba yake juu ya udhalilishaji wake wa utoto, na kujisikia kama amesalitiwa na Joseph Jackson kwa miaka mingi.[9]

Pindi ambapo anamwona Michael, anakuwa hana furaha kibisaa; Jackson alielezea, "Hata nikiuwa nyumbani, Nakuwa mpweke. Huwa ninakaa chumbani kwangu na kuanza kulia. Ni vigumu sana kuwa na marafiki ... Kuna kipindi pia natembelea majirani nyati za usiku, nikiwa na matumani ya kumpata japo mtu wa kuongea naye. Lakini inaishia nikiwa narudi nyumbani."[10]

Kurekodi

hariri

Jackson akaungana tena na mtayarishaji wa abamu ya Off the Wall Quincy Jones ili kurekodi albamu ya sita. Wawili hao walifayanyakazi pamoja katika nyimbo takriban 300  tisa katika hizo zikabahatika kuingizwa kwenye albamu. Thriller ilirekodiwa kati ya mwezi wa Aprili na Novemba kwenye mwaka wa 1982, ikiwa na bajeti ya dola za Kimarekani zipatazo 750,000. Wanachama kadhaa wa bendi ya Toto nao walishiriki katika kurekodi za albamu hii.[11] Jackson ametunga nyimbo nne kwa ajili ya rekodi: "Wanna Be Startin' Somethin'", "The Girl Is Mine" (akiwa na Paul McCartney), "Beat It" na "Billie Jean". Ipo tofauti kidogo na wasanii wengine, Jackson hajaindika nyimbo hizi kwenye karatasi. Badala yake, akajirekodi kwenye kimashine cha kurekodia sauti; pale walipokuwa wanarekodi alikuwa akiimba kutoka kichwani mwake tu kwa kuwa alikuwa keshaweka kumbukumbu kichwani.[12]

Mahusiano ya baina ya Jackson na Jones yakawa mazuri mno wakati wa kurekodi albamu. Jackson ametumia muda wake mwingi wa kufanya mazoezi ya kucheza akiwa peke yake. Pale nyimbo tisa za albamu zilipomalizika, wote wawili, yaani Jones na Jackson walikuwa hawana furaha na matokeo ya kurejea kila wimbo (kufanya remix zake), walitumia wiki nzima katika kila wimbo mmoja. Jones aliamini kwamba "Billie Jean" haukuwa wimbo mkali kivile na kuwekwa pamoja kwenye albamu, lakini Jackson hakubaliana na hilo na kupelekea kuuweka kwenye albamu. Jones akamweleza Jackson kwamba Thriller isingeuza vizuri kama jinsi ilivyofanya Off the Wall, kwa sababu kwa kipindi hata soko lenyewe lilikuwa dhaifu mno. Matokeo yake, Jackson akatishia kufuta wazo la kutoka kwa albamu hii

Jackson aliunda albamu kwa kuwa alikuwa akiamini kwamba "kila wimbo ni mkali," kama jinsi alivyofanya Tchaikovsky na kazi yake ya The Nutcracker, na kutengeneza albamu ya Thriller kwa mtazamo huo.[13][14] Jones a mtunzi wa nyimbo Rod Temperton walitoa maelezo yao juu ya kilichotokea katika toleo la pili la albamu la mwaka wa 2001. Jones alijadili kuhusu "Billie Jean" na kwa nini Jackson aliichukua jambo hili kama binafsi sana, ambaye katahabika na idadi kubwa ya mashabiki wenye unyonge. Jones alitaka pale mwanzoni mwa wimbo kufupishwe; lakini, Jackson akang'ang'ania pabakie kwa sababu kumefanya aweze kucheza.[15]

Kwa kufuatia utata uliokuwa ukiendelea dhidi ya mtindo wa disco umepelekea kubadilisha mwelekeo mwingine wa muziki ili isiwe ya disko zito kama vile ilivyokuwa katika Off the Wall. Jones na Jackson wakadhamiria kutengeneza wimbo wa rock ambao utakata lufaa na kutumia mawiki kadhaa na kuanza kumtafuta mpiga gitaa mzuri aliyeweza kufanya kwa ajili wimbo wa "Beat It", wimbo ambao Jackson ametunga na kupiga ngoma zake. Kwa bahati, wakampata Eddie Van Halen wa bendi ya rock ya Van Halen.[15][16]

Wakati Rod Temperton ametunga wimbo wa "Thriller", alinuia kabisa auite "Starlight" au "Midnight Man" lakini ukabaki katika "Thriller" kwa sababu alihisi jina lingekuwa na nguvu ya kibiashara zaidi. Daima anamtaka mtu maarufu amalizie kutaja maishairi ya mwishoni, ndiyo Temperton akamleta mwigizaji Vincent Price, ambaye alimalizia sehemu yake kwa michukuo miwili tu. Temperton ametunga kisehemu cha kuongea akiwa kwenye taxi kuelekea studio. Jones na Temperton walisema kwamba baadhi ya rekodi ziliachwa kumaliziwa kwa sababu hawakuwa na mapambo tena kwa ajili ya nyimbo za albamu nyingine.

Muziki

hariri

Kwa mujibu wa Steve Huey wa Allmusic, Thriller imesafisha uwezo wa albamu iliyopita ya Jackson, Off the Wall; dansi na nyimbo za rock zenyewe zilikuwa za fujo mno, wakati tuni na ballad zilikuwa laini na za hisia kali. Nyimbo kali ambazo zimejumlisha ballad ni pamoja na "The Lady in My Life", "Human Nature", na "The Girl Is Mine"; vipande vya funk ni "Billie Jean" na "Wanna Be Startin' Somethin'"; na seti ya disco ni "Baby Be Mine" na "P.Y.T. (Pretty Young Thing)".[17][18][19] "1982 na ina milio sawa na maujanja yaliwemo kwenye Off The Wall. Wimbo unasindikizwa na besi na ngoma nzuri kwa nyuma kipande cha kati, kuna sauti inapanda kidogo ambayo ina maneno ya Kiswahili, na kuipa wimbo ladha ya kimataifa.[20] "The Girl Is Mine" inaelezea kuhusu marafiki wawili wanaogombania mwanamke, wakibishana kuwa nani anampenda zaidi na kuishiana kwa mazungumzo ya rap.[16][20]

Licha ya kuwa na ladha ya pop laini katika rekodi hizi mbili, Thriller, imezidi sana kuliko hata Off the Wall, inaonyesha vitu vikali vijavyo na chembechembe za uhusika ambao Jackson angeutumia katika kazi zake za baadaye.[21] Akiwa na Thriller, Jackson ameweza kuanzisha jumuia yake yenye athira na mandhari ya kutisha na mitazamo ya nguvu za giza, yaani, mambo ya majini-majini. Haya yameshuhudiwa kwenye nyimbo kama vile "Billie Jean", "Wanna Be Startin' Somethin'" na "Thriller".[17] Katika "Billie Jean", Jackson anaimba kuhusu mshabiki ambaye anamtuhumu kwamba amezaa naye mtoto; kwenye "Wanna Be Startin' Somethin'" anabishana na masuala ya umbye na vyombo vya habari.[18] Wimbo unaanza na besi refu na ngoma. Katika wimbo wa "Thriller", vionjo vya sauti kama vile vya mlango kufunguka, ngurumo ya radi, miguu inayosikika ikitembea kule mitini, upepo na milio ya mbwa inaweza kusikika.

Kundi la kupambana na vurugu la katika "Beat It" limekuwa heshima kubwa kwa West Side Story, na ndiyo ulikuwa wimbo wa kwanza wa Jackson kupata mafanikio makubwa kabisa kwa staili ya rock cross-over.[22][23] Baadaye Jackson alielezea kuhusu "Beat It", "suala ni kwamba hakuna mtu yoyote kuwa yeye ndiyo kidume, unaweza ukakaa mbali na ugomvi na bado ukawa mwanaume. Huna haja ya kuwa ili kuhakiki kama wewe ndiyo kidume". "Human Nature" ni wimbo wa hisia kali na kianzio cha adabu.

Kunako miaka ya 1970, uwezo wa uimbaji wa Jackson ulikuwa ukitazamika vyema sana; Allmusic walimwelezea kama "mwimbaji aliyeneemeshwa bila kutazama". Rolling Stone wanaifananisha sauti yake na mkongwe Stevie Wonder. Tafiti zao zilionyesha kwamba sauti ya "Jackson" ni laini kupita kiasi na nzuri ajabu. Inateleza taratibu mno na kuanza kwa sauti ya madaha". Pamoja na kutolewa kwa Thriller, Jackson angeweza kuimba taratibu—chini kabisa ya C—lakini kapendekeza kuimba sauti ya juu kwa sababu pop anayoimba yeye ina njia kibao ya kuunda staili mpya. Rolling Stone pia walitoa maoni yao juu ya Jackson kwamba alikuwa akiimba kwa "sauti ya kukubwa sana" ambayo ilikuwa ina "kiasi cha uzuni".[24] "P.Y.T. (Pretty Young Thing)", ulipendekezwa n James Ingram na Quincy Jones, na "Lady in My Life" na Rod Temperton, zote mbili zimeipa albamu mwelekeo imara wa R&B. Jackson akawa keshaanza kutafuta sauti ambayo atautumia (sauti ya kama kwi-kwi) ambayo aliendelea nayo hadi kwenye Thriller. Dhumuni la kuweka hiccup (kama kwi-kwi) ni kutaka kuleta hisia fulani; kuvutia watu, uzuni na uwoga fulani.[25]

Kutoka na mapokeo

hariri

Athira na urithi wake

hariri

Tasnia ya muziki

hariri

Blender wanamweleza Jackson kama "mkali wa muziki wa pop kwa karne ya ishirini", wakati The New York Times wametoa wazo la kwamba alikuwa "mtu wa ajabu kimuziki", na kwa maana hiyo "katika ulimwengu wa pop yeye ni wa kipekee, kuna Michael Jackson na kuna wengineo kibao".[26][27] Jackson amebadilisha tasnia ya muziki jinsi ilivyokuwa ikifanyakazi: vyote akiwa kama msanii binafsi, na kifedha pia, na kifaida kwa ujumla. Mwanasheria wake Bw. John Branca amegundua ya kwamba Jackson amefanikiwa kupata uaminifu wa hali ya juu kwenye tasnia ya muziki kwa maana hiyo: imekadiriwa kuwa $2 kwa kila albamu moja aliyouza. Matokeo yake, Jackson amepata kuvunja-rekodi ya mauzo ya juu kwenye CD, na katika mauzo ya nakala za documentary, The Making of Michael Jackson's Thriller, iliyotayarishwa na Jackson na John Landis. Documentary hiyo ili-lipiwa na MTV, imeuza nakala zaidi ya 350,000 katika miezi yake michache ya mwanzoni. Sokoni halafu ikaja kuendeshwa na ma-single kadhaa, Thriller iliinua umakini wa maalbamu kadhaa, bado vibao vyake mbalimbali vilichukuliwa kutoka kwenye albamu na kujipatia mafanikio kede wa kede.[28]

Muziki wa video na usawa kirangi

hariri

Kabla ya mafanikio ya Thriller, wengi walihisi kwamba Jackson ametaabika sana kupata kupigiwa nyimbo zake kwenye MTV kwa sababu alikuwa mtu mweusi.[29] Wakati anafanya juhudi za kupata kupigwa nyimbo za Jackson, Rais wa CBS Records Bw. Walter Yetnikoff akawasukuma MTV ili wampigie nyimbo zake na kutangaza, "Sikupi tena video yoyote ile na naenda kusema mbele ya hadhara na kudadadeki zenu na kuwaambia ukweli kwamba hamtaki kupiga nyimbo za washikaji weusi".

Nafasi yake ikatoa msukumo kwa MTV kuanza kupiga wimbo wa "Billie Jean" na baadaye "Beat It", ambayo ilileta ujamaa na baadaye kusaidia wasanii wengine weusi wa muziki kupata ule mkondo wa kufahamika.[30] MTV wamekana madai hayo ya ubaguzi wa rangi katika urushaji wa matangazo yao.[31] Umaarufu wa video zake, kama vile "Beat It" na "Billie Jean", umesaidia idhaa ndogo-ndogo "kwenye ramani", na MTV wakazingatia kujikita katika pop na R&B.[30][32]

 
Jackson katika mapinduzi ya video ya Thriller

Jackson amebadilisha ukati wa muziki wa video kwa aina ya sanaa ya uendelezaji yakinifu kwa kuweka mstari wa hadithi tata, utaratibu wa kucheza, vionjo maalumu na kuuzisha sura watu maarufu katika video zake.[22] Wakati urefu wa dakika 14 za video ya Thriller, MTV wanaipiga mara mbili kwa saa ili kufikia matakwa ya watazamaji.[33] Filamu fupi imewekewa alama ya ongezeka la uzani wa muziki wa video na ulikuwa umewekewa utaratibu wa kuitwa muziki bora wa video ambao haukuwahi kufanywa hapo awali.[34] Umaarufu kwa muziki wa video umerejesha albamu nyuma hadi kufikia kiwango cha kuwa namba moja kwenye chati, lakini studio ya Jackson haikuunga mkono toleo la tatu la wimbo wa video kutoka katika albamu. Walikuwa tayari weshalizika na mafanikio walioyapata, kwa hiyo Jackson akawashawishi MTV wamlipe kazi yake.[16][33]

Mtunzi wa vitabu, na mwandishi wa ukosoaji wa muziki Nelson George aliandika mwaka 2004, "Ni vugumu sana kusikia nyimbo kwenye Thriller na kuzitoa kwenye mavideo yake. Wengi wetu picha peke yake inaelezea wimbo. Kiukweli ingekuwa mabishano ya kwamba Michael ni msanii wa kwanza wa MTV kuwa picha kamili ya albamu yake yote na kuuteka fikra za watu kwa mtazamo wake". Filamu fupi kama Thriller inabaki kuwa kama mtindo pekee kwa Jackson, wakati mlolongo zima wa kikundi cha kucheza cha kwenye "Beat It" kimekuwa kikigezewa mara kwa mara na watu wengine.

Uchezaji wa muziki uliochezwa kwenye Thriller umekuwa utamaduni ambao mashuhuri sana ulimweunguni, umegezewa kila mahali huko India na katika majela kadhaa ya huko nchni Ufilipino.[35][36]

Kwa msanii ambaye ni mweusi kwa miaka ya 1980 kufikia kiwango hicho, mafanikio ya Jackson yalikuwa ya kipekee. Kwa mujibu wa The Washington Post, Thriller imesafisha njia ya mafanikio kwa Waafrika-Waamerika wengine kama vile Prince.[37] Wimbo wa "The Girl Is Mine" ulipata kete nyingi kwa kupata wapenzi wengi wa rangi tofauti kupitia redio, yaani, Wazungu na Weusi.[38] Gazeti la Time lilieleza, "Jackson ni kitu kikubwa sana tangu hapo The Beatles. Yeye ni msanii pekee kwa upande wa wasanii wa kujitegemea tangu hapo alipokuwa Elvis Presley. Anaweza kuwa mwimbaji maarufu sana milele kwa upande wa waimbaji Weusi".

Orodha ya nyimbo

hariri
# JinaMtunzi (wa) Urefu
1. "Wanna Be Startin' Somethin'"  Michael Jackson 6:02
2. "Baby Be Mine"  Rod Temperton 4:20
3. "The Girl Is Mine"  Jackson 3:42
4. "Thriller"  Temperton 5:57
5. "Beat It"  Jackson 4:19
6. "Billie Jean"  Jackson 4:54
7. "Human Nature"  John Bettis, Steve Porcaro 4:05
8. "P.Y.T. (Pretty Young Thing)"  James Ingram, Quincy Jones 3:58
9. "The Lady in My Life"  Temperton 4:59
"Toleo Maalumu la 2001"
# JinaMtunzi (wa) Urefu
10. "Interview with Quincy Jones #1"    2:18
11. "Someone in the Dark" (previously unreleased)Bergman/Bergman/Temperton 4:48
12. "Interview with Quincy Jones #2"    2:04
13. "Billie Jean" (demo, previously unavailable)Jackson 2:20
14. "Interview with Quincy Jones #3"    3:10
15. "Interview with Rod Temperton #1"    4:02
16. "Interview with Quincy Jones #4"    1:32
17. "Voice-Over Session from Thriller" (previously unreleased)Temperton 2:52
18. "Interview with Rod Temperton #2"    1:56
19. "Interview with Quincy Jones #5"    2:01
20. "Carousel" (previously unreleased)Sembello/D. Freeman 1:49
21. "Interview with Quincy Jones #6"    1:17

Marejeo

hariri
  • George, Nelson (2004). Michael Jackson: The Ultimate Collection booklet. Sony BMG.
  • Taraborrelli, J. Randy (2004). The Magic and the Madness. Terra Alta, WV: Headline. ISBN 0-330-42005-4.
  1. "Review: Thriller". Q (Januari 2000): 138.
  2. Rosenberg, Tal (19 Juni 2007). "Review: Thriller". Stylus Magazine. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-03-20. Iliwekwa mnamo 13 Juni 2009.
  3. "Grammy Award Winners". The Recording Academy. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-01-02. Iliwekwa mnamo 14 Februari 2008.
  4. Erlewine, Stephen. "Off the Wall Overview". Allmusic. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-09-06. Iliwekwa mnamo 15 Juni 2008. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |https://web.archive.org/web/20080906104301/http://www.allmusic.com/cg/amg.dll?p= ignored (help)
  5. Holden, Stephen. "Off the Wall : Michael Jackson", Rolling Stone, 1 Novemba 1979. Retrieved on 23 Julai 2008. Archived from the original on 2007-12-23. 
  6. "Michael Jackson: Off the Wall - Classic albums - Music - Virgin media". Virgin Media. Iliwekwa mnamo 12 Desemba 2008.
  7. Taraborrelli, p. 190
  8. Taraborrelli, p. 191
  9. Taraborrelli, p. 196
  10. Taraborrelli, p. 206
  11. Taraborrelli, pp. 220–221
  12. Taraborrelli, pp. 209–210
  13. Ebony Magazine: Michael: 25 Years After Thriller, Desemba 2007, pg. 97–98
  14. Jackson, Michael. Interview with Jesse Jackson. Machi 2005.
  15. 15.0 15.1 Jackson, Michael. Thriller Special Edition Audio.
  16. 16.0 16.1 16.2 "Michael Jackson's Monster Smash". The Daily Telegraph. 25 Novemba 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-04-29. Iliwekwa mnamo 20 Aprili 2008. {{cite web}}: Italic or bold markup not allowed in: |publisher= (help)
  17. 17.0 17.1 Erlewine, Stephen (19 Februari 2007). "Thriller Overview". Allmusic. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-09-06. Iliwekwa mnamo 15 Juni 2008. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |https://web.archive.org/web/20080906104301/http://www.allmusic.com/cg/amg.dll?p= ignored (help)
  18. 18.0 18.1 Connelly, Christopher (28 Januari 1983). "Michael Jackson: Thriller". Rolling Stone. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-06-22. Iliwekwa mnamo 15 Juni 2008. {{cite web}}: Italic or bold markup not allowed in: |publisher= (help); Unknown parameter |= ignored (help)
  19. Henderson, Eric (2003). "Michael Jackson: Thriller". Slant Magazine. Iliwekwa mnamo 15 Juni 2008. {{cite web}}: Italic or bold markup not allowed in: |publisher= (help)
  20. 20.0 20.1 Taraborrelli, pp. 223–225
  21. Pareles, Jon. "Critic's Notebook; How Good Is Jackson's 'Bad'?", The New York Times, Septemba 1987. Retrieved on 19 Aprili 2007. 
  22. 22.0 22.1 Huey, Steve. "Michael Jackson - Biography". Allmusic. Iliwekwa mnamo 11 Novemba 2006.
  23. "Michael Jackson: Biography". The New Rolling Stone Album Guide. 2004. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-02-20. Iliwekwa mnamo 14 Februari 2008. {{cite web}}: Italic or bold markup not allowed in: |publisher= (help); Unknown parameter |= ignored (help)
  24. Connelly, Christoper. "Michael Jackson: Thriller", Rolling Stone, 28 Januari 1983. Retrieved on 23 Julai 2008. Archived from the original on 2008-06-22. 
  25. George, p. 22
  26. "Michael Jackson, "Billy Jean"". Blender. 2005. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-03-12. Iliwekwa mnamo 11 Aprili 2007. {{cite web}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
  27. "Michael Jackson At 25: A Musical Phenomenon", The New York Times, Januari 1984. Retrieved on 15 Mei 2007. 
  28. "Michael Jackson". VH1. 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-03-05. Iliwekwa mnamo 22 Februari 2007.
  29. "Michael Jackson, "Billy Jean:". Blender. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-03-12. Iliwekwa mnamo 11 Aprili 2007. {{cite web}}: Italic or bold markup not allowed in: |work= (help)
  30. 30.0 30.1 Gundersen, Edna (25 Agosti 2005). "music videos changing places". USA Today. Iliwekwa mnamo 6 Aprili 2008. {{cite web}}: Italic or bold markup not allowed in: |publisher= (help)
  31. "Why it took MTV so long to play black music videos | Jet | Find Articles at BNET". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-25. Iliwekwa mnamo 2012-05-25.
  32. "Why Are Michael Jackson's Fans So Devoted?". ABC News. 23 Februari 2005. Iliwekwa mnamo 6 Aprili 2007.
  33. 33.0 33.1 Taraborrelli, pp. 270–271
  34. "Michael Jackson". VH1. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-03-05. Iliwekwa mnamo 22 Februari 2007.
  35. "1500 Prisoners Perform Thriller Dance". The Wrong Advices. 21 Julai 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-02-10. Iliwekwa mnamo 5 Aprili 2008.
  36. "Jacko goes bollywood". TMZ.com. 3 Oktoba 2006. Iliwekwa mnamo 8 Aprili 2008.
  37. Harrington, Richard. "Prince & Michael Jackson: Two Paths to the Top of Pop", The Washington Post, Oktoba 1988. Retrieved on 21 Mei 2007. Archived from the original on 2007-10-11. 
  38. Christgau, Robert. "Robert Christgau: Artist 932". Robert Christgau.com. Iliwekwa mnamo 27 Juni 2008.