Wasandawe ni kabila linaloishi hasa katika eneo la wilaya ya Chemba, mkoa wa Dodoma, katikati ya nchi ya Tanzania.

Picha ya eneo la sandawe

Wasandawe katika wilaya ya Chemba wanaishi hasa katika tarafa mbili, yaani Farkwa na Kwamtoro.

Wengi ni wafupi na wa rangi ya weupe/njano. Wanawake wana maumbo ya kuvutia na wanaume wana muonekano wa pekee.

Asili na uenezi hariri

Mpaka mwaka 2012 kabila hilo la pekee lilionekana katika vipimo kuwa na viini nasaba vya zamani kuliko makabila yote duniani[1].

Kinasaba ndugu zao wa jirani ni hasa Wakhoisan wa Kusini mwa Afrika (Botswana, Namibia, Afrika Kusini na Angola. Wanajulikana kama "watu wa kwanza" na ndio wenyeji wakongwe zaidi kusini mwa Afrika. Wakaguzi na wageni wametazama kwa watu wa Bushmen kwa dalili za jinsi wanadamu walivyoweza kuishi katika Zama za Mawe), halafu Waethiopia.

Mwaka 2000 idadi ya Wasandawe ilikadiriwa kuwa 40,000 [2], na mwaka 2013 60,000, wengi wao wakiwa Wakristo, hasa Wakatoliki.

Lugha hariri

Lugha yao ni Kisandawe, ya jamii ya Kikhoisan: ina fonimu nyingi kuliko lugha zote duniani, zikiwa ni pamoja na "click sounds". Inafikiriwa kuwa ya zamani kuliko zote, kwa kuwa inafanana bado na zile za wenzao Kusini mwa Afrika, ingawa walitengana miaka 40,000 hivi iliyopita. Inasemekana ni lugha tamu isiyochosha kusikiliza.

Utamaduni hariri

Miaka ya nyuma wengi wao walikuwa hawajasoma bali sasa wanasomesha vijana wao, hasa baada ya kuanzishwa shule za kata kama Farkwa Secondary, Kwamtoro Secondary, Makarongo Secondary, Gwandi Secondary, Kurio Secondary n.k.

Vilevile Wasandawe wengi wanajihusisha na kilimo japo bado wanaendelea na uwindaji, kwa kuwa chakula chao cha asili ni nyama.

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • Bauer, Andreus. "Street of Caravans"
  • Iliffe, John. "A Modern History of Tanganyika"
  • "Mankind, the Illustrated Encyclopedia of" Pub. Marshall Cavendish
  • Prince, Tom von. Gegen Araber und Wahehe
  Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wasandawe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.