Wilaya ya Chemba
Chemba ni jina la wilaya mpya katika mkoa wa Dodoma, Tanzania yenye postikodi namba 41800[1], ambayo ilianzishwa rasmi mnamo Machi 2012 kwa kumega wilaya ya Kondoa[2].
Wilaya ya Chemba | |
Mahali pa Chemba mkoani Dodoma | |
Majiranukta: 05°14′34″S 35°53′24″E / 5.24278°S 35.89000°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mikoa | Mkoa wa Dodoma |
Idadi ya wakazi (2022) | |
- Wakazi kwa ujumla | 339,333 |
Jiografia
haririWilaya ya Chemba inapakana na wilaya ya Kondoa upande wa kaskazini, mkoa wa Manyara upande wa mashariki, wilaya ya Chamwino na wilaya ya Bahi upande wa kusini, na mkoa wa Singida upande wa magharibi.
Makao makuu ya wilaya yako Chemba.
Wakazi
haririKadiri ya sensa ya mwaka 2012, wilaya ya Chemba ilikuwa na wakazi 235,711.[3] Katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 339,333 [4].
Wakazi wengi wa Chemba ni wakulima na wafugaji na mazao yao ni kama vile mahindi, ulezi, alizeti, uwele, udo. Wanyama wanaofugwa ni kama vile ng'ombe, mbuzi, punda na kondoo.
Chemba ni miongoni mwa sehemu ambazo zipo nyuma sana kielimu, pia eneo hili lina shida kubwa ya maji katika vijiji vyake vyote.
Usafiri
haririBarabara T5 kutoka Dodoma hadi Babati inapitia wilaya hii.[5]
Ugatuzi
haririKwa sasa Wilaya ya Chemba inajumuisha tarafa za Goima, Mondo, Kwamtoro na Farkwa pamoja na kata zake 26.[3]
Kata
hariri
|
Tanbihi
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2020-03-21. Iliwekwa mnamo 2017-10-08.
- ↑ "New constituencies up for grabs as CUF cries foul". The Citizen. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-20. Iliwekwa mnamo 21 Julai 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 "Census 2012". National Bureau of Statistics. Iliwekwa mnamo 21 Julai 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ "Dodoma Roads Network" (PDF). Tanroads. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 24 Juni 2016. Iliwekwa mnamo 17 Juni 2016.
{{cite web}}
: Unknown parameter|deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Kata za Wilaya ya Chemba - Mkoa wa Dodoma - Tanzania | ||
---|---|---|
Babayu | Chandama | Chemba | Churuku | Dalai | Farkwa | Goima | Gwandi | Jangalo | Kidoka | Kimaha | Kinyamsindo | Kwamtoro | Lahoda | Lalta | Makorongo | Mondo | Mpendo | Mrijo | Msaada | Ovada | Paranga | Sanzawa | Songolo | Soya | Tumbakose |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Dodoma bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Chemba kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |